Maandamo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoani Simiyu yaliyofanyika wiki iliyopita. (Picha Maktaba) |
Watendaji wa Mahakama wakiwemo mahakimu wa Mahakama mbalimbali za Mkoa wa Simiyu, wakiwa kwenye hafla ya Kilele cha maazimisho ya Wiki ya Sheria nchini. |
Watendaji wa Mahakama wakiwemo mahakimu wa Mahakama mbalimbali za Mkoa wa Simiyu, wakiwa kwenye hafla ya Kilele cha maazimisho ya Wiki ya Sheria nchini. |
Na Derick Milton, Bariadi.
Imeelezwa kuwa kutokana na juhudi za serikali
inazozifanya za kuweka mazingira mazuri na wezeshi ya Biashara na uwekezaji
nchini na kuvutia wawekezaji wengi, hali hiyo imesababisha ongezeko la migogoro
ya kibiashara na binafsi.
Kutokana na hali hiyo imeshauliwa migogoro hiyo kumalizwa
kwa njia ya usuruhishi, ili kuweza kupata utatuzi wa haraka, kwa gharama nafuu,
na wenye haki ili kuweza kukuza uchumi wa nchi.
Hayo yamesemwa leo na Hakimu mkazi mfawidhi
Mahakama ya Mkoa wa Simiyu Martha Mahumbuga kwenye maazimisho ya kilele cha
wiki ya sheria nchini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mahakama ya Mkoa.
Amesema kuwa kuwepo wa mazingira mazuri ya
ufanyaji biashara kwa sasa nchini, na kuweza kuvutia wawekezaji wengi,
imesababisha na migogoro ya kibiashara kuongezeka.
Amesema kuwa ni vyema wahusika kwenye migogoro
hiyo kutumia njia ya usuruhishi kama njia sahihi na bora ya kuendeleza uchumi wa
nchi na wa mmoja mmoja kwani njia hiyo ni rafiki kwa pande zote.
“ Ni ukweli usiopingika kuwa uchumi wa nchi yetu unaendelea
vizuri na umefanyika kuwa endelevu …na hii imepelekea kuvutia wawekezaji wengi
kuja nchini, na biashara kuwepo,” amesema Mhe: Mahumbuga
“ Kutokana na hali hiyo ya uwekezaji na biashara
nchini, ni bayana kwamba kuna ongezeko la migogoro ya kibiashara na Binafsi, hivyo ni bora
kutumia njia ya usuruhishi ili kuwa na utatuzi wa haraka, na gharama nafuu, na
wenye haki kwa migogoro ya kibiashara na kila inapowezekana ili uchumi uendelee
kukua haraka,”
Amesema kuwa lengo la mahakama kuwataka wananchi
kutumia njia ya usuruhishi kwenye migogoro yao ni kutaka kuwa na jamii yenye
amani, furaha na upendo.
MWISHO.
Post a Comment