Na Mwandishi wetu, Bariadi.
Leo kupitia (simiyupresstz.blogspot.com) tumeripoti juu ya kunaswa kwa kiwanda Bubu
kilichokuwa kikitengeneza pombe kali aina ya Konyagi, kiwanda ambacho
kimekamatwa katika Mtaa wa Budeka, kata ya Sima Wilaya ya Bariadi Mkoani
Simiyu.
Kiwanda hicho kilibainika baada ya
Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya
ya Bariadi kufanya opereisheni na kukuta vijana wakiendelea na utengenezaji wa
pombe hiyo kwenye nyumba moja iliyoko katika mtaa huo.
Hata hivyo wahusika wa kiwanda
hicho bubu, walikodi moja ya nyumba katika mtaa huo na kuanza kungeneza pombe
hiyo ambayo inadaiwa kutokuwa salama kwa walaji.
Hivi ndivyo pombe hiyo ilivyokuwa ikitengenezwa.
Taarifa zinaeleza kuwa bidhaa
hiyo ilikuwa ikizalishwa kienyeji licha ya kuwa na nembo halali ya Konyagi,
stika za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), lakini pia bidhaa hiyo haina tarehe
ya kuanza kutumika wala tarehe ya mwisho wa matumizi (Expire date).
Mbali na hilo pombe hiyo
inadaiwa ilikuwa ikitengenezwa kwa kuchanganywa Maji na Spriti, ambapo wahusika
walikuwa wakitafuta chupa tupu za konyagi, maboksi yenye nembo ya Konyagi,
kisha kufanya mchanyiko na kupeleka sokoni.
Akizungumzia tukio hilo, kwa
niaba ya Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala wilaya ya Bariadi Nichodemus Shirima
amesema wamekamata watu wawili waliokuwa katika kiwanda hicho bubu huku
akibainisha kuwa pombe ambayo ilikuwa ikitengenezwa kwenye kiwanda hicho ni
hatari kwa walaji.
“Hiki kinywaji hakijapimwa,
hakina TBS, hakuna mtu anayejua kama kinywaji hiki ni sumu au laah…inaonekana
kuna ulegevu katika ukaguzi mpaka watu wameamua kuanzisha viwanda bubu katika
makazi ya watu lakini tunashukuru hatimaye wamebainika’’ amesema na kuongeza.
Post a Comment