SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limeshauri Uwanja wa Benjamini
Mkapa uliopo jijini Dar es Salaam kutotumika kwenye mechi zao kwa kile
kilichoelezwa kuwa umeharibika eneo la kuchezea (pitch), ambapo sasa utafungwa
kwa mwezi mmoja kupisha marekebisho.
Hivyo basi, baada ya mechi ya leo Jumatano ya Ligi Kuu Bara kati
ya Yanga na KMC, itakayochezwa kuanzia saa 10:00 jionib uwanja huo utafungwa.
Kwa mujibu wa matumizi ya uwanja huo, unapaswa kutumika mara tatu
kwa wiki lakini hadi leo itakuwa ni mara ya nne kinyume na matumizi ya uwanja
huo ambao hata kabla ya hapo ulilalamikiwa kutokuwa katika hali nzuri hasa eneo
la kuchezea (pitch), kwani matumizi yamekuwa makubwa.
Tangu Jumamosi iliyopita, uwanja huo ulianza kutumika na Simba
walipoikaribisha Raja Casablanca mechi yao ya pili ya hatua ya makundi ya Ligi
ya Mabingwa Afrika ikifungwa mabao 3-0.
Siku iliyofuata, Yanga nao waliikaribisha TP Mazembe mechi ya pili
ya Kombe la Shirikisho Afrika ikishinda mabao 3-1.
Baada ya mechi hizo za CAF, jana Jumatatu kulikuwa na mechi ya
Ligi Kuu Bara, Simba ilicheza na Azam usiku kuanzia saa 1:00 na leo ni KMC na
Yanga ambapo zitakuwa zimebaki siku tatu kufikisha wiki moja, hivyo matumizi
yamezidi.
Akizungumza na Mwanaspoti, Meneja wa Uwanja huo, Salum Mtumbuka
alisema kuwa baada ya mechi mbili za CAF zilizochezwa wikiendi iliyopita
walikutana na maofisa hao ambao waliwapa maelekezo namna ya kufanya marekebisho
hasa eneo la kuchezea.
"Tulikubaliana kwa pamoja na Caf kwamba wakati marekebisho
yanaendelea ambayo yatachukua muda wa mwezi mmoja, mechi zitakazochezwa hapo
hapo labda ni zile za kimataifa za CAF na timu ya Taifa, mechi zingine za ligi
kuu wanaotumia uwanja huu watatafuta viwanja vingine hata Uhuru upo.
"Simba na Yanga ndiyo wanaotumia huu uwanja kama uwanja wao
wa nyumbani, ila ndani ya kipindi cha marekebisho haya hawatatumia mechi zao za
Ligi Kuu kwenye uwanja huu, tunawapa Uwanja wa Uhuru ama watakavyoona
nao," alisema na kuongeza;
إرسال تعليق