Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mashimba Ndaki. |
Na Derick Milton, Bariadi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Maswa Magharibi Mkoani Simiyu Mashimba Ndaki ameuomba uongozi wa Mkoa
huo, kutafakari upya juu ya katazo lake la Magari madogo (Michomoko) kutofanya
kazi ya kusafirisha abiria ndani ya mkoa huo.
Kauli hiyo ya Waziri nakuja zikiwa zimepita wiki
mbili tangu Chama cha mapinduzi (CCM) mkoani huo, kuutaka pia uongozi wa Mkoa
kutafakari upya katazo hilo kwani limeadhiri ajira za vijana wengi.
Julai 13, 2022 aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo David
Kafulila, aliweka zuio la magari hayo kufanya kazi ya kusafirisha abiria ndani
ya mkoa huo, hiyo ni baada ya kutokea ajali mbili mfulululizo na kusababisha
vifo vya watu 10 na majeruhi 17 ndani ya siku 12.
Wakati akipiga
marufuku magari hayo, Kafulila alisema kuwa yalikuwa yakifanya kazi kinyume cha
utaratibu wa leseni zao, huku akibainisha kuwa yalikuwa yakipakia abiria hadi
11 wakati uwezo wake ni abiria watano.
Jana kwenye kikao cha
kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) Waziri ndani akichangia mada mbalimbali,
aliomba uongozi wa mkoa kukaa kwa mara nyingine na kutafakari zuio hilo kama
bado lina tija kwa ajira za vijana au hapana.
Ndaki alisema kuwa
magari hayo yalikuwa yameajiri vijana wengi, ambao kwa sasa wamebaki bila ajira
baada ya marufuku hiyo, huku akitaka kutafutwa njia mbadala ya kuzuia ajali
lakini magari hayo yaendeleee kufanya kazi.
Alisema kuwa serikali
inazo njia nyingi na zenye kuwezesha kuzuia ajali za mara kwa mara Barabarani
kutokana na kuwa na vyombo vingi vya kupambana na jambo hilo.
“ Hata tukiangalia
kwa sasa ajali bado zinaendelea kutokea, mimi nafikiri tunaweza kukaa meza moja
tena na wahusika wa magari haya, tukatafuta njia sahihi ya kuzuia ajali na siyo
kuzuia wafanye kazi” alisema Ndaki….
“ Kuendelea kuzuia
magari haya vijana wengi wanaendelea kuteseka uko mitaani, hawana ajira na hii ndiyo
ilikuwa ajira yao, walijiajiri wenyewe, na kazi hii ilikuwa halali siyo kwamba
ilikuwa haramu, kama ilikuwa halali na wana leseni, wanalipia mapato kwanini
wazuiwe?”
Alisema kuwa ni vyema
yakawepo makubaliano kwa pande zote husika, ya jinsi ya kukomesha ajali na
kuwekeana masharti ya ubebaji abiria ili vijana waendelee kufanya kazi na
kujiingizia kipato.
Akizungumzia jambo
hilo Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahya Nawanda ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho alisema
kuwa, hata yeye alikuta zuio hilo hivyo atakaa na kamati yake ya ulinzi na
usalama kuweza kulijadili upya jambo hilo.
Nawanda alisema kuwa
hadi kufikia uhamuzi huo, jambo hilo lilianzia kwenye kamati hiyo, hivyo lazima
alirudishe uko uko kujadiliwa upya kama ambavyo Waziri ameshauli kwani ndicho
chombo chake kikuu cha kumshauri.
“ Chombo changu
kikubwa cha kunishauli ni kamati ya ulinzi na usalama, Mheshimiwa Waziri
tumepokea ushauli wako na tutakwenda kuufanyia kazi na kamati yangu, kisha
tutakuja na majibu” alisema Nawanda.
MWISHO.
إرسال تعليق