COWOCE Yahamasisha Utoaji Chakula kwa Wanafunzi Shuleni


Mwenyekiti wa COWOCE B, Mosi Rashid (aliyevaa ushungi) na Mwenyekiti wa COWOCE A Magdalena Yohana (aliyevaa nguo ya zambarau) na  Mkurugenzi wa COWOCE, Joseph Ndatala (mwenye nguo nyeupe kulia) wakikabidhi mchele kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Ndala (kushoto). Wa pili kulia ni  Mwakilishi wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndala, James Samwel.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Vikundi vya wanawake wanaojihusisha na ujasiriamali vilivyojengewa uwezo na Shirika lisilo la Kiserikali la Companion of Women and Children Empowerment (COWOCE) la Mjini Shinyanga vimehamasisha wazazi kutoa chakula kwa ajili ya wanafunzi shuleni wawe na lishe nzuri ili kuongeza ufaulu kwenye mitihani.


Vikundi hivyo viwili vya akina mama ambavyo ni COWOCE A na COWOCE B vimetoa elimu ya uhamasishaji utoaji chakula shuleni leo Jumatano Machi 1,2023 katika shule ya Sekondari Ndala iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga wakati vikikabidhi chakula kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu.

Awali akizungumza, Mkurugenzi wa Shirika la Kiserikali lisilo la Companion of Women and Children Empowerment (COWOCE) ambaye ni Mwenyekiti wa Wazazi shule ya Sekondari Ndala bw. Joseph Ndatala amesema ni jukumu la wadau wote kuhakikisha wanahamasisha wazazi waweze kuchangia chakula shuleni.

“Utafiti unaonesha wazi kuwa mtoto ambaye amekwenda shule ya awali anafanya vizuri sana shuleni lakini unaambatana na kuwa mtoto anayekula shuleni anafanya vizuri sana darasani kuliko mtoto ambaye hali. Kama mtoto anaingia darasani saa mbili asubuhi mpaka saa 11 jioni hajala kamwe hawezi kumsikiliza vizuri mwalimu”,ameeleza Ndatala

“Tumekuja hapa tukiambatana na Vikundi vya COWOCE A na B vinavyosimamiwa na shirika letu la COWOCE linalojihusisha na haki za wanawake na watoto na kuwajengea uwezo wa kujiajiri vijana.

Lengo kubwa siyo kuja kutoa msaada bali lengo kubwa sana ni kufikisha ujumbe kwa wazazi wenu na walezi wenu kwamba wana wajibu wa kutoa chakula shuleni. Watoto wengine wapo kwenye mazingira magumu lakini haiwezekani mnakosa hata 1,000/= au 4000/= ya chakula kwa mtoto”,amesema Ndatala.


Amewasihi wanafunzi kuzungumza na wazazi na walezi wao watoe chakula shuleni ili wasome kwa utulivu, wawe la lishe nzuri na kufanya vizuri kwenye mitihani.


“Hakuna mtoto asiyekula chakula nyumbani, sasa kama watoto wote tunakula chakula nyumbani usiku, naomba tupeleke ujumbe kwa wazazi wachange chakula angalau kidogo kidogo ili muweze kusoma vizuri tupate Mawaziri humu, Wabunge, Madiwani wanaotoka shule zetu kwa sababu chakula kinaongeza afya. Ili tuwe na lishe bora lazima tule chakula”,amesema Ndatala.
“Hapa tumekuja na chakula kidogo ambacho kwa niaba yenu wanafunzi wachache watapokea hicho chakulaIkiwa ni sehemu ya kuhamasisha utoaji wa chakula shuleni, wazazi watoe chakula na nyinyi watoto msome shule. Pia tunampatia chakula (Mchele kilo 22) mwanafunzi mmoja wa shule ya Sekondari Masekelo kw ajili ya kula shuleni. Hapa katika shule ya Sekondari Ndala tumeleta kilo 30 za mchele”,ameongeza Ndatala.


Aidha amewataka wanafunzi kuzingatia masomo yao na kuepuka vishawishi na wahakikishe wanapokutana na shida barabarani au popote watoe taarifa kwa mama, baba , mwalimu au kiongozi yeyote.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa COWOCE A Magdalena Yohana ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la TAG Eden Tembo Ndala amewataka wanafunzi hao kumtumaini Mungu katika maisha yao akisisitiza kuwa kuwa katika mazingira magumu isiwe sababu ya kukatiza masomo hivyo kuwasihi kutokubali kukatishwa tamaa.


Naye Mwenyekiti wa COWOCE B, Mosi Rashid amewaomba wazazi na walezi kutoa chakula kwa wanafunzi ili kuongeza ufaulu kwenye mitihani yao lakini pia kuhakikisha watoto wanakuwa na afya bora.


Mjumbe wa COWOCE A, Happy Mathias amewataka wanafunzi kuacha kujiingiza kwenye masuala ya mapenzi kwani yanachangia mimba za utotoni na wajiepushe na magenge yasiyofaa yakiwemo ya watumiaji wa dawa za kulevya.
Kwa upande wao wanafunzi hao wameishukuru COWOCE kwa kuhamasisha wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi hali itakayosaidia wanafunzi kuwa na utulivu shuleni.


Mwakilishi wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndala, James Samwel ambaye ni Mwalimu wa Taaluma wa shule hiyo, amesema mara baada ya kukaa kwenye kikao na wazazi walibaini kuwa wapo baadhi ya wanafunzi wanashindwa kupata chakula shuleni kutokana na kwamba wanatoka kwenye mazingira magumu hivyo kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia chakula kwa watoto wanaotoka kwenye mazingira magumu lakini pia kila mmoja kuwa balozi wa kuhubiri utoaji chakula shuleni.

Hata hivyo amesema Shule ya Sekondari Ndala imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani kutokana na kwamba inatoa huduma ya chakula kwa wanafunzi shuleni.
Mwenyekiti wa COWOCE B, Mosi Rashid (aliyevaa ushungi) na Mwenyekiti wa COWOCE A Magdalena Yohana (aliyevaa nguo ya zambarau) na  Mkurugenzi wa COWOCE , Joseph Ndatala (mwenye nguo nyeupe kulia) wakikabidhi mchele kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Ndala (kushoto). Wa pili kulia ni  Mwakilishi wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndala, James Samwel. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa COWOCE B, Mosi Rashid (aliyevaa ushungi) na Mwenyekiti wa COWOCE A Magdalena Yohana (aliyevaa nguo ya zambarau) na  Mkurugenzi wa COWOCE, Joseph Ndatala (mwenye nguo nyeupe kulia) wakikabidhi mchele kwa mwanafunzi wa shule ya sekondari Masekelo (kushoto).
Mwenyekiti wa COWOCE B, Mosi Rashid (aliyevaa ushungi) na Mwenyekiti wa COWOCE A Magdalena Yohana (aliyevaa nguo ya zambarau) na  Mkurugenzi wa COWOCE (mwenye nguo nyeupe kulia) wakikabidhi mchele kwa mwanafunzi wa shule ya sekondari Masekelo (kushoto).
Mwenyekiti wa COWOCE A Magdalena Yohana akizungumza katika Shule ya Sekondari Ndala Manispaa ya Shinyanga wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.
Mwenyekiti wa COWOCE B, Mosi Rashid akizungumza katika Shule ya Sekondari Ndala Manispaa ya Shinyanga wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.
Mkurugenzi wa COWOCE, Joseph Ndatala akizungumza katika Shule ya Sekondari Ndala Manispaa ya Shinyanga wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.
Mkurugenzi wa COWOCE, Joseph Ndatala akizungumza katika Shule ya Sekondari Ndala Manispaa ya Shinyanga wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.
Mkurugenzi wa COWOCE, Joseph Ndatala akizungumza katika Shule ya Sekondari Ndala Manispaa ya Shinyanga wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.
Mkurugenzi wa COWOCE, Joseph Ndatala akizungumza katika Shule ya Sekondari Ndala Manispaa ya Shinyanga wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.
 Mwakilishi wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndala, James Samwel akizungumza katika Shule ya Sekondari Ndala Manispaa ya Shinyanga wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.
Mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Masekelo akizungumza katika Shule ya Sekondari Ndala Manispaa ya Shinyanga wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.
Mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Ndala akizungumza katika Shule ya Sekondari Ndala Manispaa ya Shinyanga wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.
Mjumbe wa COWOCE A, Happy Mathias akizungumza katika Shule ya Sekondari Ndala Manispaa ya Shinyanga wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.
Mjumbe wa COWOCE B, Annamarry Joseph Kasenga akizungumza katika Shule ya Sekondari Ndala Manispaa ya Shinyanga wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.
Wajumbe wa COWOCE na wanafunzi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.
Wajumbe wa COWOCE na wanafunzi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.
Wajumbe wa COWOCE na wanafunzi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.

Wajumbe wa COWOCE na wanafunzi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.

Wajumbe wa COWOCE na wanafunzi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa uhamasishaji wazazi kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni.
Wajumbe wa COWOCE A na B na Mkurugenzi wa Shirika la COWOSE , Joseph Ndatala wakipiga picha ya kumbukumbu katika shule ya Sekondari Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Wajumbe wa COWOCE A na B na Mkurugenzi wa Shirika la COWOSE , Joseph Ndatala wakipiga picha ya kumbukumbu katika shule ya Sekondari Ndala Manispaa ya Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post