Wajumbe wa Umoja wa Wanawake (UWT) wilaya ya Busega wakiimba nyimbo kabla ya kuanza mkutano wa UWT wilayani humo.
Katibu wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Simiyu Mondester Mwaya akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani).
Na COSTANTINE MATHIAS, Busega.
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Simiyu Ester Midimu amewataka Wanawake mkoani humo kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi anazozifanya za kuwaletea maendeleo wananchi.
Amesema Rais anaendelea kutekeleza miradi katika sekta za Elimu, Afya, Maji, Umeme na Barabara kwa kujenga Madarasa ya kisasa, vituo vya afya na zahanati.
Ameyasema hayo leo wilayani Busega, wakati akifanya mahojiano maalumu na waandishi wa Habari kuelekea siku ya Wanawake duniani yatakayofanyika Machi 8, 2023 kimkoa wilayani Meatu.
Midimu amesema Rais Samia ameleta fedha nyingi kwenye miradi mbalimbali ambapo wanawake wanaendelea kunufaika ikiwemo miradi ya maji iliyowatua wakina mama ndoo kichwani.
‘’Ametele fedha nyingi kwenye miundombinu ya Elimu, Afya, Maji, Umeme na Barabara…wanawake tunatakiwa kumuunga mkono Rais Samia kwa sababu madarasa mazuri yamejengwa kila mahali, vituo vya afya kila mahali’’ amesema Midimu na kuongeza.
‘’natoa wito kwa wanawake wa mkoa wa Simiyu kumuunga mkoa Rais Samia kwa sababu anatekeleza Ilani ya CCM…tumejipanga kuhamasisha wanawake ili wajitokeze kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake’’.
Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Simiyu Mondester Mwaya amesema watahakikisha wanayatangza mema na mazuri yote yanayofanywa na Rais Samia kupitia mikutano ya hadhara na vikao vya ndani.
Kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani, Katibu huyo amesema UWT mkoa huo imejipanga vizuri kuwatembelea wanawake wote katika wilaya zote za Mkoa wa Simiyu.
‘’Tutaenda kila wilaya kukutana na wanawake ili kumsemea Rais Samia kwa yale anayoyafanya kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kushika dola…tuko bega kwa bega na Rais Samia ametutendea haki CCM’’ amesema Katibu huyo.
MWISHO.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
Post a Comment