Muonekano wa Soko la Bariadi, Mkoani Simiyu kwa ndani. |
Na
Derick Milton, Simiyu.
Taasisi ya kuzuia na kupamba na Rushwa (TAKUKURU)
Mkoa wa Simiyu imesema kuwa vibanda vingi kwenye masoko ya Halmashauri za
Wilaya ya Maswa, Meatu na Bariadi vinamilikiwa na viongozi.
Aidha taasisi hiyo imesema kuwa baadhi ya viongozi
wanamiliki vibanda zaidi ya kimoja kwenye masoko hayo na kuvitumia kwa
kujinufaisha wenyewe tofauti na malengo ya serikali ya kuwasaidia wafanyabishara
wadogo na wale wa kati.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za
taasisi hiyo kwa miezi mitatu kwa waandishi wa habari leo Naibu Mkuu wa
Takukuru Mkoa Aron Missanga, amesema kuwa uchunguzi walioufanya umebaini kuwa
viongozi hao walitumia madaraka yao vibaya kwa kuhodhi vibanda hivyo.
“ Tulichobaini ni kuwa baadhi ya viongozi ndiyo
wamiliki wa vibanda hivyo, tena wanamiliki vibanda viwili hadi vitatu, kisha
wanawapangisha wafanyabishara kwa bei kubwa, na wanalipa kiasi kidogo kwenye
halmashauri huku wakichukua kiasi kikubwa kwa wafanyabishara”….
“ Lengo la serikali kujenga masoko haya ni
kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wao wapate sehemu za kufanyabiashara wajipatie
kipato kwa gharama nafuu, lakini hilo haliko hivyo kwenye masoko yetu, vibanda
vingi vimehodhiwa na viongozi,” amesema Missanga.
Naibu Mkuu huyo wa Takukuru amesema kuwa katika
uchunguzi wa mfumo wa upangishaji wa masoko hayo, baada ya kubaini jambo hilo
waliwaita wamiliki wa soko ambao ni halmashauri kwa ajili ya kulitafutia
ufumbuzi.
Amesema kuwa baada ya kuwaita wamiliki, walikaa
kikao na kufanya mazungumzo kisha kuweka maazimio, ambayo ameeleza Halmashauri
wametakiwa kwenda kuyafanyia kazi kadri walivyokubaliana.
Katika hatua nyingine taasisi hiyo imesema kuwa
ndani ya pindi hicho jumla ya kesi 8 ambazo ilizifikisha mahakamani na kutolewa
uhamuzi, kati ya hizo 7 takukuru ilishinda huku ikishindwa kesi moja.
Taasisi hiyo imesema kuwa hatua hiyo ni mafanikio
makubwa ambayo imepata, kutokana na umahili na ubora wa waendesha mashtaka
waliopo kwenye taasisi hiyo lakini pia kufanyika uchunguzi ulio bora.
MWISHO.
Post a Comment