Serikali yawatoa hofu wanachi mvutano wa Soko na Stendi.

Wananchi wa Kijiji cha Nyahanga, Kata ya Nyashimo wilayani Busega Mkoani Simiyu wakiwa kwenye mkutano kwa ajili ya kuiomba serikali kuwarejeshea Soko na Stendi zinazotarajiwa kujengwa kujengwa Lamadi.


Wanawake Wakiwa kwenye Mkutano uliofanyika kijiji cha Nyahanga, kata ya Nyashimo wilayani Busega.


Viongozi wa Kamati ya Kufuatilia Stendi na Soko kutoka kijiji cha Nyahanga, kata ya Nyashimo wilayani Busega wakiwa kwenye mkutano kwa ajili ya kutoa taarifa kwa wananchi wa kijiji hicho.



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Yahaya Nawanda.

Eneo liliotengwa kwa ajili ya stendi katika Kata ya Nyashimo wilayani Busega Mkoani Simiyu.


Na COSTANTINE MATHIAS, Busega.

 

SERIKALI Mkoani Simiyu imewataka Wananchi wa Kata ya Nyashimo wilayani Busega, mkoani humo kuwa watulivu na wavumilivu kuhusu ahadi ya Rais Samia aliyoitoa mwaka jana juu ya kuwajengea stendi pamoja na soko.

 

Rais Samia akiwa katika Mji wa Lamadi wilayani Busega, wakati akielekea kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliwaahidi wananchi kuwa atawajengea Soko na Stendi.

 

Akizungumza ofisini kwake juzi, Mkuu wa Mkoa huo Dk. Yahaya Nawanda alisema Rais Samia ameshaleta mchakato kwa ajili ya kuleta fedha hizo, lakini kuna sintofahamu kati ya wananchi wa Lamadi na Nyashimo.

 

Alisema Nyashimo ni makao makuu ya wilaya ya Busega na Lamadi ni mji mdogo kwenye wilaya hiyo ambapo wananchi wa Lamadi waliomba stendi na Soko kwa Rais Samia.

 

‘’Niwambe wananchi wa Nyashimo, serikali inatoa kwa kupanda mahitaji kwa muda, safari hii wanapata hawa na safari nyingine wanapata wengine…ile ilikuwa ni ahadi ya Rais Samia, ni lazima tuitekeleze, niwaombe wananchi wa Nyashimo tayari tuna mipango na waokupata soko la kisasa’’ alisema Dk. Nawanda.

 

Alisema serikali haiwezi kupeleka vitu vyote kwa wakati mmoja, lakini pia rasilimali haziwezi kujitosheleza kupeleka miradi mingi inayofanana katika wilaya moja.

 

Leokadia Pamba, Mkazi wa Nyang’hanga, kijiji cha Bulima, kata ya Nyashimo alisema kilio kikubwa cha wananchi wa Nyashimo ni kupata stendi na soko lakini wilaya hiyo haina soko wala stendi na badala yake inataka kujengwa nje ya makao makuu ya wilaya kwenye mji mdogo wa Lamadi.

 

Alisema wananchi wa Nyashimo walitoa eneo kwa ajili ya maandalizi ya stendi ikiwemo kuhamisha makaburi, lakini wanashangaa stendi na soko vinataka kujengwa Lamadi.

 

‘’stendi na soko tunanyang’anywa, mama Samia utuone sisi wananchi wa Nyashimo…stendi inajengwa Lamadi, hata makao makuu yalitaka kuondolewa hapa…’’ alisema Zuhura Ramadhani, Mkazi wa Nyahanga.

 

Naye Haji Matiku, mkazi wa kijiji cha Bulima alisema walishapeleka barua ya Malalamiko kwa Mkuu wa wilaya ya Busega, lakini wilaya hiyo inakwamishwa na wana siasa kuchelewesha maendeleo.

 

Alisema kijiji hicho kilitoa maeneo kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu ya wilaya ya Busega ikiwemo maeneo ya ujenzi wa stendi na soko, lakini wanashangaa kuona soko na stendi vinajengwa mji wa Lamadi.

 

Yusuph Kijika, mkazi wa Kijiji cha Nyashimo alisema kijografia, waliamua Nyashimo kuwa makao makuu ya wilaya na kwamba eneo hilo ni katikati ya wilaya ya Busega, lakini wanashangaa kukosa stendi na soko.

 

Akisoma malalamiko yao, Sospeter Ndalo alisema Lamadi walikishwa pelekewa stendi kwa gharama za stendi lakini haikufanya kazi hadi sasa ni magofu, na kwamba mji wa Lamadi una masoko mawili ya Senta na Lukungu.

 

Aliongeza kuwa wameamua watafute haki ili soko na stendi zijengwe makao makuu ya wilaya ya Busega yaliyoko Nyashimo kuliko kujenga Lamadi ambayo ni nje ya mji na kwamba Nyashimo ni rahisi kwa wananchi kuja kupata huduma katikakati ya Wilaya.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kufuatilia Soko na Stendi aliyechaguliwa na wananchi Thomas Chenge alisema wanaendelea kufuatilia kurejeshewa stendi na soko ili kuhakikisha yanajengwa makao makuu ya wilaya hiyo Nyashimo.

 

‘’2011/2012 baada ya kutangaziwa kuwa tumepewa Halmashauri kutoka Magu, nayo ilipindishwa ikapelekwa Igalukilo, wengine wametangulia mbele ya haki…na hili linataka kuporwa na watu wachache, ninyi wananchi ndio wenye wilaya, hatuwezi kukubali stendi na soko viondolewe hapa’’ alisema Chenge.

 

Aliwataka wananchi hao kuendelea kushikamana ili kuhakikisha ahadi ya Rais Samia inatekelezwa makao makuu ya wilaya, wakati huo wameshafikisha kilio cha kwa viongozi wa ngazi za wilaya na Mkoa. 

 

MWISHO.

 

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post