MBUNGE KUNDO AMWAGA MABATI 276, PAMPU ZA MAJI, JEZI NA MIPIRA KATA YA MWADOBANA.

 



Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew amekabidni mabati 276 na mifuko 45 ya saruji  kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa vya Shule za Msingi Byuna, Mwabuluda, Mwabuki pamoja na ofisi ya Kijiji cha Mwabuluda ili kuunga Mkono jitihada za Serikali kuendeleza sekta ya Elimu.


Katika hatua nyingine, Mbunge huyo pia amekabidhi pampu za Maji kwa kila vijiji vya Byuna, Ikungulyandili, Mwabuluda na Mwadobana kata ya Byuna wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo leo, wakati akiwasilisha Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM), Mhandisi Kundo amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo katika kata hiyo ikiwemo kuwekeza katika Elimu kwa kuboresha miundombinu yake.



"Tunapoboresha maisha, tunapamba na umaskini kwa Vitendo, tumeleta minara ya mawasiliano, Umeme, Barabara na makalavati ili wananchi wajiinue kiuchumi hata mtu mmojammoja...Tukiboresha sekta ya Afya tunapambana na Maradhi, tumewekeza katika miundombinu ya Elimu na kupata Walimu kuendana na mahitaji ya Sasa, ili kuondoa ujinga." Amesema Mhandisi.


Ameeleza kuwa atahakikisja anaboresha kila sekta, ili wananchi wawe na maisha bora pia serikali ya Dk. Samia imeondoa michango ya kuchangia ujenzi wa miundombinu katika sekta za Elimu, Afya na Maji.

Katika hatua nyingine m, Mbunge huyo amekabidhi vifaa vya michezo ikiwemo mipira minne kwa kila kijijiji na jezi pea moja kila Kijiji huku kata ya Mwadobana ikikabidhiaa jezi pea moja na mipira mitatu.


"Tumekuja na mipira na jezi kila Kijiji kitapata ambapo Mwadobana watapata jezi pea moja na mipira minne, Ikungulyandili jezi na mipira minne, Byuna jezi na mipira minne na Mwabuluda jezi na mipira minne hivyo tutaacha Mipira 19 na jezi seti 5" amesema Mhandisi Kundo.

Awali Diwani wa Kata ya Mwadobana, Duka Mashauri amesema Ilani ya CCM katika kata hiyo Imetekelezwa kwa asilimia 100 huku akiwapongeza watumishi wa Umma kwa Usimamizi mzuri wa miradi ya Maendeleo.


Mwisho.





















Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post