Mwenyekiti wa Jicho la Tanzania mkoa wa Shinyanga,
ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini, Oscar Kaijage (kulia) akimkabidhi tisheti yenye nembo ya Jicho la Tanzania Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda.
Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
MKUU wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda amesema atahakikisha anashirikiana na Taasisi ya Jicho la Tanzania pamoja na mashirika mengine ya kiraia ili kuendelea kuisaidia serikali kusukuma gurudumu la maendeleo.
Amesema mashirika hayo yamekuwa yakiisaidia serikali kuunga mkono jitihada za maendeleo kwenye sekta za afya, kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia, mmomonyoko wa maadili na wanayo nafasi ya kuisemea serikali.
Dk. Nawanda ameyasema hayo leo ofisini kwake, wakati akizungumza wa viongozi wa taasisi hiyo waliofika ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha, kukabidhi chati cha utambuzi na hati ya usajili.
Amesema mashirika ya kijamii yanaishi na wananchi moja kwa moja, hivyo wanao wajibu wa elimisha jamii kuhusu mmomonyoko wa maadili pia wamekuwa sehemu ya kuiisemea serikali.
‘’Jicho la Tanzania wamejipambanua kuizungumza serikali na kueleza yale yanayotekelezwa, kazi yao kubwa ni sisi tusiposema wao watatukumbusha kwa wananchi yaliyofanywa na serikali’’ amesema Dk. Nawanda na kuongeza.
‘’Niwapongeze Jicho la Tanzania, nami naahidi nitawapa ushirikiano kwa asilimia 100, wana lengo moja tu la kuhubiri mazuri yanayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita...kwa pamoja tukishirikiana tutafika mbali sana.
Katika hatua nyingine Dk. Nawanda ameyataka mashikika ya kiraia kufanya kazi kwa mujibu wa usajili na vibali vyao huku akionya kuwa hataki kuona mambo ya ushoga, ulawiti na ukatili wa kijinsia kuwa hayana nafasi Mkoa wa Simiyu.
Mwenyekiti wa Jicho la Tanzania mkoa wa Shinyanga, ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini, Oscar Kaijage amesema taasisi hiyo ina viongozi nchi nzima kwa ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya, kata na Vijiji.
Amesema taasisi hiyo imeanzishwa kwa ajili ya kuwasemea viongozi wa Chama na Serikali kwenye jamii kwa mzuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Jicho la Tanzania Mkoa wa Simiyu Farida Suleiman Hemed amesema wajipanga kuhakikisha kuwasemea viongozi wa kitafa, mikoa, wilaya pamoja na Chama cha Mapinduzi.
Ameongeza kuwa wajipanga kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto, vijana, wanawake na pia watahakikisha wajikita katika utunzaji wa mazingira ili kuwa na mazingira endelevu.
MWISHO.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com


Post a Comment