Katika hali isiyokuwa ya kawaida Ofisa Utumishi mmoja ambaye
alihudumu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kwa
kushirikiana na Afisa kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii PSSF wanaida kuchezea
mfumo na kusataafisha watumishi wa serikali kabla ya muda.
Licha ya Maafisa hao kitendo hicho, mtumishi huyo
alilipwa Milioni 72 kama mafao yake baada ya kustaafishwa, jambo la kinyama na
la kuumiza zaidi ulifanywa mchezo na taasisi moja ya kifedha iliyokuwa inamdai
mtumishi huyo ambapo alikatwa kiasi Cha Sh. Milioni 70, na kumbakizia kiasi cha
Sh. Milioni 2.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda leo kwenye kikao
cha Baraza maalumu la Madiwani Halmashauri ya Mji wa Bariadi la kujadili hoja
za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG), ndiye ameeleza jambo
hilo.
Dkt. Yahaya Nawanda amesema kuwa kitendo hicho ni cha
kinyama, ambapo ameagiza Maafisa hao kutafutwa popote walipo hata kama
wamehamishwa na amehaidi kupambana nalo hadi hatua kali zichukuliwe dhidi yao.
Amesema kuwa Maafisa hao walikuwa wanachezea mfumo
wa utumishi, ambapo mtumishi anashtukia anapigiwa simu kuwa anastaafu jambo
ambalo siyo kweli, lengo likiwa ni kutaka kujipatia fedha kwa njia haramu.
“Huyu Afisa utumishi na afisa wa PSSF baada ya kufanikiwa
kumstaafisha, huyu mtumishi kuna kampuni moja ya kifedha ilikuwa inamdai,
wakala njama, akaingiziwa penshioni yake Milioni 72, walichomfanyia ni kitu cha
kinyama, wakamtaka Milioni 70 akabaki na Milioni mbili tu” amesema Nawanda….
“ Nimeagiza uchunguzi uanze mara moja, tunakwenda kuunda tume
tuchunguze jambo hili, lakini huyu Afisa Utumishi na Afisa wa PSSF watafutwe
popote walipo waje hapa watueleze kwani nini walifanya jambo hili,” ameeleza
Nawanda.
MWISHO.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
Post a Comment