MWENGE WA UHURU; Kuzindua miradi miradi ya zaidi ya Bil. 15 Simiyu.


Mwenge wa Uhuru.

 

 

Na Mwandishi Wetu.

 

Mwenge wa Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka 2023/24 unatarajiwa kupokelewa Mkoani Simiyu Julai 21, 2023 na utazindua miradi ya zaidi ya Shilingi Bil. 15 Mkoani Simiyu, Mkuu wa Mkoa huo Dk. Yahaya Nawanda ameeleza.

 

Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 zinaongozwa na kaulimbiu inayosema Tunza mazingira,okoa vyanzo vya Maji kwa ustawi wa viumbe hai.

 

Akizungumza na Wananchi 17 Julai 2023 kupitia Studio ya Redio Nyanza FM Dkt. Nawanda amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa Mkoani Simiyu kwa Takribani Siku 6 kuanzia Tarehe 21  Julai 2023 utakapopokelewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega  hadi Tarehe 27  ambapo utakabidhiwa Mkoani Shinyanga.

 

Ameitaja miradi itakayozinduliwa kuwa ni pamoja na Miundombinu ya Barabara,Miradi ya Maji,Miradi ya kuhamasisha Lishe,Klabu za kupinga Rushwa pamoja na madawa ya kulevya,pamoja na Miradi mbalimbali ya Sekta binafsi kikiwemo Kituo cha Redio Nyanza FM.

 

Dkt.Nawanda ametoa rai kwa Wananchi kushiriki kikamilifu katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru  pamoja  na kushiriki kikamilifu katika Shughuli zote za Mwenge wa Uhuru katika kipindi chote utakapokuwepo  Mkoani Simiyu.

 

MWISHO.

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم