UWT yatoa siku 90 kukamilisha mradi wa Maji.

Meneja Ufundi kutoka MAUWASA Mhandisi Leonard Mnyeti (mwenye t-shirt nyeupe katikati) akisoma taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa Tanki la Maji kijiji cha Hinduki wilayani Maswa, kulia ni MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) na MNEC, Zainabu Shomari pamoja na Mbunge wa Vijana Mkoa wa Simiyu Lucy Sabu.


Na COSTANTINE MATHIAS, Maswa.

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) na MNEC, Zainabu Shomari ameitaka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (MAUWASA) wilayani Maswa Mkoani Simiyu kuhakikisha wanakamilisha mradi wa maji ndani ya siku 90.

 

Aidha, ameitaka Mamlaka hiyo kutoa taarifa mbele ya Viongozi wa serikali na Chama Cha Mapinduzi kama mradi huo umeshindwa kutekelezeka kutokana na ukosefu wa fedha.

 

Hayo yamebianishwa leo na Makamu huyo alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani kwa kutembelea mradi wa maji unatokelezwa na Mamlaka hiyo katika kijiji cha Hinduki wilayani humo kwa gharama ya shilingi Bil. 2.2.

 

Amesema hajaridhishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao umelenga kuwahudumia wananchi baada ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia kuahidi kuwatua akina mama ndoo kichwani.

 

‘’kama kuna tatizo lolote ambalo mnahisi linaleta mkwamo, hiki ni Chama Cha Mapinduzi na serikali yetu na viongozi ni wasikivu…hatupendelei kuona na kusikia kuna mkwamo wa mradi wa maji kwa kukosa fedha’’ amesema na kuongeza.

 

‘’Rais Samia amehakikisha analeta fedha kwa ajili ya kumtua mama ndoo kichwani, mnaona maeneo yote ya Tanzania yanafaidika…mkisema changamoto ni fedha, ninakuwa sielewi hasa katika suala la maji’’

 

Amefafanua kuwa wananchi hawaridhiki kuona tanki la maji limejengwa kwa muda mrefu na halikamiliki ambapo aliwataka viongozi kusimamia mradi huo unakamilika ndani ya miezi mitatu ili wananchi waweze kunufaika.

 

Amewataka Viongozi wa MAUWASA kuwashirikisha viongozi wa Chama na serikali ili waweze kuweka msukumu kwa ajili ya kupata fedha za kukamilisha mradi huo ambapo waathirikia wakubwa wa ukosefu wa maji ni wanawake.

 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohamed amesema mradi huo unahitajika kwa wananchi ili kuwaondolea adha ya upatikanaji wa maji katika mji wa Maswa.

 

‘’Kama tatizo ni fedha, tushirikisheni Chama ili tuweze kuongeza nguvu kusukuma kupata fedha…tuliahidi kwa wananchi kufikisha asilimia 80 ya upatikaji wa maji vijijini, kusuasua kwa utekelezaji wake ni changamoto kwetu’’ amesema Shemsa.

 

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo Meneja Ufundi kutoka MAUWASA Mhandisi Leonard Mnyeti amesema ujenzi wa mradi huo unatekelezwa kwa ghamara ya shilingi Bil. 2.2 na umefikia asilimia 65.

 

Amesema mradi huo unakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa fedha na kwamba unatekelezwa kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma na kupunguza gharama za umeme kutoka shilingi Mil. 30 hadi shilingi Mil. 24.

 

MWISHO.

 

Tanki lenye ujazo wa lita Mil. 2 linalojengwa kwa gharama ya shilingi Bil. 2.2 na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (MAUWASA) katika kijiji cha Hinduki wilayani Maswa Mkoani Simiyu.


Meneja Ufundi kutoka MAUWASA Mhandisi Leonard Mnyeti (mwenye t-shirt nyeupe katikati) akisoma taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa Tanki la Maji kijiji cha Hinduki wilayani Maswa, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) na MNEC, Zainabu Shomari pamoja na Mbunge wa Vijana Mkoa wa Simiyu Lucy Sabu, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoani humo Shemsa Mohamed.

 

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) na MNEC, Zainabu Shomari akitoa maelekezo mara baada ya kukagua ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita mil. 2.2 kijiji cha Hinduki wilayani Maswa.

 

 

 

 

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم