Na COSTANTINE MATHIAS, Meatu.
SERIKALI ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi Bil. 8 kwa ajili ya kujenga daraja la Mto Itembe wilayani Meatu Mkoani Simiyu ili kurahisisha mawasiliano, usafiri na usafirishaji wa bidhaa.
Awali mto huo ulikuwa kikwazo cha Mawasiliano na Usafiri baina ya Wilaya za Meatu na Mkalama Mkoani Singida ambapo wananchi wameipongeza serikali kwa kunusuru maisha yao kwa kusombwa na maji.
Wametoa pongezi mbele ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Simiyu kukagua ujenzi huo, wamesema miaka ya nyuma mifugo na binadamu walikuwa wanapoteza maisha nyakati za masika kwa kusomba na maji na pia kukwama kusafiri kutokana na mto huo kujaa maji.
‘’Tunaishukuru serikali ya Dk. Samia kwa kutujengea daraja hili, hakika tumeona matunda ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi…tunaishukuru serikali imetukomboa kwa kujenga daraja la Mto Itembe’’ amesema Matei Mashauri.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo shemsa Mohammed alimpongeza Raisa Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Barabara na madaraja.
Amesema awali mto huo ulikuwa changamoto kwa wananchi wa Wilaya ya Meatu na maeneo jirani kwa kusababisha vifo ambapo alimtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kukamilisha kwa wakati ili wananchi wanufaike.
‘’Mto huu ulikuwa unakata mawasiliano, niaombe tu
likamlishwe kwa wakati…kila mkandarasi anayetekeleza mradi anaacha madeni kwa
vibarua na mamalishe…meneja wa TANROADS hakikisha mkandarasi huyu haachi madeni
kwa vibarua kwa sababu serikali inatoa fedha ya kutekeleza mradi husika,
hakikisheni hakuna madeni yanayobakia baada ya mkandarasi kukamilisha mradi.'' amesema Shemsa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda alimhakikishia Mwenyekiti wa CCM kuwa watahakikisha wanasimamia utekelezaji wa mradi huo ikiwemo kumsimamia mkandarasi anayetekeleza miradi huo.
Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Simiyu Mhandisi Raphael Chasama amesema daraja hilo litagharimu shilingi Bilioni 8 na pia ni kichocheo cha uchumi na mawasiliano kwa wananchi wa Wilaya za Meatu na Mkoa wa Singida.
Amefafanua kuwa mradi huo umefikia asilimia 63 ambapo ujenzi wa nguzo umekamilika wakati huo serikali imeshamlipa mkandarasi kiasi cha shilingi Bilioni 2.
MWISHO.
Ujenzi wa daraja la Mto Itembe ukiendelea.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
Post a Comment