
Naibu
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Simiyu Aron Missanga akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za taasisi hiyo mjini Bariadi.
Na
Derick Milton, Simiyu.
Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU)
imesema kuwa katika kipindi cha Julai hadi Septemba, 2023 imebaini Halmashauri
za Mkoa wa Simiyu haziwasilishi kodi ya zuio katika Mamlaka ya mapato (TRA) kama
sheria inavyotaka.
Takukuru imeeleza kuwa katika uchunguzi wa mifumo ya
ukataji na uwasilishaji wa kodi ya zuio ambao ilifanya zaidi ya Milioni 50
zimebainika hazijawasilishwa TRA na Halmashauri licha ya watoa huduma kukatwa
kodi hiyo.
Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa Aron Missanga akizungumza
na waandishi wa habari leo, amesema kuwa Halmashuari ziliwakata kodi hiyo watoa
huduma, lakini hazijawasilisha sehemu inakotakiwa kuwasilishwa (TRA).
“Sheria inasema kuwa mtu yeyote anayetoa huduma kwenye
taasisi za serikali, mfano kujenga zahanati, madarasa au kituo cha Afya, wale
wanaoleta vifaa vya ujenzi lazima wakatwe kodi ya zuio,”….
“ Tulichobaini ni kuwa hiyo kodi watao huduma wanakatwa
kama sheria inavyotaka, na Halmashauri ndiyo wanawakata, sasa tatizo lipo kwa
halmashauri yenyewe kuwasilisha hiyo kodi TRA, tumebaini zaidi ya Milioni 50
hazijawasilishwa mpaka sasa,”
Aidha amesema kuwa katika uchunguzi huo, walibaini
wahusika wanaotakiwa kukata kodi hiyo hawana uelewa wa jinsi ya kuwasilisha
kodi hiyo TRA, lakini pia wanatekeleza miradi wengi hawana namba mlipakodi (TIN
Number).
“ Aidha tulibaini kitengo cha kutoa elimu Mamlaka ya
mapato (TRA) Mkoa wa Simiyu bado hakijatekeleza wajibu wake wa kuhakikisha
kinatoa elimu kwa wahusika ili kuhakikisha wanapata uelewa wa kutosha wa jinsi
ya kulipa kodi hiyo.
Missanga amesema kuwa katika kuhakikisha sheria hiyo
inatekelezwa waliitisha mkutano na wadau wote, zikiwemo halmashauri na TRA na
kuwekeana mikakati ya kuhakikisha kodi hiyo inalipwa na wahusika wanapewa
elimu.
Katika hatua nyingine TAKUKURU katika kipindi hicho
imeweza kufuatilia miradi 24 ya maendeleo yenye thamani ya Sh. Bilioni 8.8 kwa
lengo la kudhibiti ubadhirifu na kuhakikisha thamani halisi ya fedha iliyotolewa
inapatikana.
Katika Miradi hiyo taasisi hiyo ilibaini baadhi yake
kuwa na mapungufu katika maeneo ya ujenzi, usimamizi na manunuzi, ambapo
wahusika walipewa taarifa ya kuhakikisha inarekebishwa kwa mujibu wa taratibu
zilizowekwa.
MWISHO.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
Post a Comment