TAKUKURU: Halmashauri Simiyu hazijalipa kodi ya zuio TRA zaidi ya Milioni 50.

Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Simiyu Aron Missanga akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za taasisi hiyo mjini Bariadi.



Na Derick Milton, Simiyu.


Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) imesema kuwa katika kipindi cha Julai hadi Septemba, 2023 imebaini Halmashauri za Mkoa wa Simiyu haziwasilishi kodi ya zuio katika Mamlaka ya mapato (TRA) kama sheria inavyotaka.


Takukuru imeeleza kuwa katika uchunguzi wa mifumo ya ukataji na uwasilishaji wa kodi ya zuio ambao ilifanya zaidi ya Milioni 50 zimebainika hazijawasilishwa TRA na Halmashauri licha ya watoa huduma kukatwa kodi hiyo.


Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa Aron Missanga akizungumza na waandishi wa habari leo, amesema kuwa Halmashuari ziliwakata kodi hiyo watoa huduma, lakini hazijawasilisha sehemu inakotakiwa kuwasilishwa (TRA).


“Sheria inasema kuwa mtu yeyote anayetoa huduma kwenye taasisi za serikali, mfano kujenga zahanati, madarasa au kituo cha Afya, wale wanaoleta vifaa vya ujenzi lazima wakatwe kodi ya zuio,”….


“ Tulichobaini ni kuwa hiyo kodi watao huduma wanakatwa kama sheria inavyotaka, na Halmashauri ndiyo wanawakata, sasa tatizo lipo kwa halmashauri yenyewe kuwasilisha hiyo kodi TRA, tumebaini zaidi ya Milioni 50 hazijawasilishwa mpaka sasa,”


Aidha amesema kuwa katika uchunguzi huo, walibaini wahusika wanaotakiwa kukata kodi hiyo hawana uelewa wa jinsi ya kuwasilisha kodi hiyo TRA, lakini pia wanatekeleza miradi wengi hawana namba mlipakodi (TIN Number).


“ Aidha tulibaini kitengo cha kutoa elimu Mamlaka ya mapato (TRA) Mkoa wa Simiyu bado hakijatekeleza wajibu wake wa kuhakikisha kinatoa elimu kwa wahusika ili kuhakikisha wanapata uelewa wa kutosha wa jinsi ya kulipa kodi hiyo.


Missanga amesema kuwa katika kuhakikisha sheria hiyo inatekelezwa waliitisha mkutano na wadau wote, zikiwemo halmashauri na TRA na kuwekeana mikakati ya kuhakikisha kodi hiyo inalipwa na wahusika wanapewa elimu.


Katika hatua nyingine TAKUKURU katika kipindi hicho imeweza kufuatilia miradi 24 ya maendeleo yenye thamani ya Sh. Bilioni 8.8 kwa lengo la kudhibiti ubadhirifu na kuhakikisha thamani halisi ya fedha iliyotolewa inapatikana.


Katika Miradi hiyo taasisi hiyo ilibaini baadhi yake kuwa na mapungufu katika maeneo ya ujenzi, usimamizi na manunuzi, ambapo wahusika walipewa taarifa ya kuhakikisha inarekebishwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.


MWISHO.


Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم