Mbunge Ester Midimu amwaga Baiskeli, Majiko ya Gesi kwa viongozi UWT.


 MAjiko ya Gesi yaliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Simiyu Ester Midimu.


Baiskeli zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu Ester Midimu ili kuwasaidia viongozi wa UWT kuwafikia wana CCM ngazi ya Kata, Vijiji na Matawi.


Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

 

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu Ester Midimu ametoa Baiskeli 450 na majiko ya Gesi 450 kwa viongozi wa kata kupitia Umoja wa Wanawake (UWT) wa mkoa huo ili kuwawezesha kufanya kazi za Chama Cha Mapinduzi na kutunza mazingira.

 

Mbunge huyo amesema wanawake hao wamekuwa sehemu ya uhamasishaji kwa wapiga kura, kutafuta kura za Chama cha Mapinduzi, kuhamasisha daftari la wapiga kura na kwamba jiografia ya mkoa wa Simiyu siyo rafiki, hivyo ameamua kuwapatia baiskeli ili ziweze kuwasadia kutafuta kura za Dk. Samia.

 

Midimu ameyasema hayo jana kwenye kikao cha Baraza la UWT lililofanyika katika ukumbi wa CCM mjini Bariadi ambapo amesema pamoja na kuwapatia usafiri pia ametoa majiko ya gesi kwa kila mmoja ili kuwaondolea adha ya kutafuta kuni na mkaa.

 

Amesema katika uwezeshaji wanawake kiuchumi, ametoa zaidi ya shilingi mil. 45 ili kuwezesha vikundi vya wanawake ili wajikwamue kiuchumi kwa kuongeza mitaji katika biashara zao na waweze kujiongezea vipato.

 

‘’Natoa baiskeli 450 na majiko 450 yenye thamani ya shilingi Mil. 230 kwa wakina mama kupitia Umoja wa wanawake, tuendelee kumuunga mkono Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye tangu aingie madarakani amejenga hospitali tatu ndani ya mkoa wa Simiyu katika wilaya za Busega, Itilima na Bariadi’’ amesema Ester.

Ameongeza kuwa serikali ya Dk. Samia imeboresha hospitali, vituo vya afya, na zahanati kwa kutoa vifaa tiba na madawa ili kuimarisha utoaji wa huduma za afya.

 

Mbunge huyo amewataka wanawake kuendelea kuhamasisha wanawake wenzao ili wajitokeze kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa (2024) na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani 2025 huku akiwasisitiza kuchagua viongozi wanaotokana na CCM.

 

Awali Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Simiyu Mariam Manyangu amewataka wanawake hao kuwa mstari wa mbele kukipigania Chama Cha Mapinduzi ili kiendelee kuwa madarakani.

 

Amewataka kufanya kazi kwa bidii katika ngazi za vijiji na kata kutafuta wanachama wapya ili kuongeza kura za Dk. Samia Suluhu Hassan na kwamba Umoja wa Wanawake wamejipanga kumchukulia fomu ya kugombea Urais Dk. Samia ikifika 2025.

 

MWISHO.

 

Wajumbe wa Baraza la UWT Mkoa wa Simiyu.

 

Wajumbe wa Baraza la UWT Mkoa wa Simiyu.

 

Wajumbe wa Baraza la UWT Mkoa wa Simiyu.


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu Ester Midimu akiwa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Simiyu Mariamu Manyangu.


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu Ester Midimu (kushoto), Kulia ni Katibu wa UWT Mkoa wa Simiyu Mondester Mwaya, katikati ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Simiyu Mariamu Manyangu.
 

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu Ester Midimu (kushoto), Kulia ni Katibu wa UWT Mkoa wa Simiyu Mondester Mwaya, katikati ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Simiyu Mariamu Manyangu, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la UWT mkoa huo.
 

Mjumbe wa Baraza la UWT Taifa Christina Chenge akiwapungia mkono wajumbe wa Baraza la UWT mkoa wa Simiyu (hawapo pichani).


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda (wa tatu kulia) akishiriki kukabidhi baiskeli zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa huo Ester Midimu (mwenye kaniki nyekundu).


Baiskeli zilizotolewa na Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Simiyu Ester Midimu.


Ugawaji wa Majiko ukiendelea.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu Ester Midimu akikabidhi fedha kwa viongozi wa UWT Mkoa  huo, Kulia ni Katibu wa UWT Mkoa wa Simiyu Mondester Mwaya, katikati ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Simiyu Mariamu Manyangu.

 

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Simiyu Mariamu Manyangu akiwasalia wajumbe wa Baraza la UWT Mkoa .
 
 

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم