Waliofariki Machimbo ya Bariadi Waagwa, Majina Yatajwa.

Kaimu Kamanda wa Zimamoto mkoa wa Simiyu Faustine Mtitu akitoa taarifa ya majina ya wachimbaji waliofariki dunia baada ya kufukiwa na udongo katika mgodi wa Ikinabushu juzi.


Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

 

KUFUATIA vifo vya watu 22 walifukiwa na udongo Januari 13, 2024 katika mgodi wa Ikinabushu wilayani Bariadi, Serikali Mkoani Simiyu imesema zoezi la kutambua na kuchukua miili ya marehemu iliyokuwa imehifadhiwa katika hospitali ya Mji wa Bariadi Somanda na Hospitali ya Mkoa wa Simiyu Nyaumata linaendelea.

 

Akitoa taarifa hizo leo mbele ya waandishi wa Habari, Kaimu Kamanda wa Zimamoto mkoa wa Simiyu Faustine Mtitu amewataja waliopoteza maisha kwa kufukiwa na mgodi huo ambao wote ni wanaume, kuwa ni Dwasi Ndaki (28), Magembe Sitta (30), Musa Shinyanga (32), Sono Sayi (33), Mshona Mbona (41) na Tuyi Nhandi (34).

 

Wengine ni Kichiba Masunga (24), Ngamba Inuka (21), Makolo Nyanghumbu, Doto Weda, Kuhoka Chacha (33), Mayala Maendeleo (35), Komeja Maduhu (29), Sayi Zanzibar (20), Doya Kiluma, kija Lubala, Kimeli Chokozi (39), Joeli Matiku 26, Maduhu Nsungi, Toroti Gregori (32), Jumanne Sondihi na kilindo Nyamhanda (44).

 

Ameongeza kuwa miili iliyokuwa imeopolewa katika mgodi huo baadhi yao taarifa na umri wao bado haujapatikana na kwamba wanaendelea kufuatilia ili kupata taarifa kwa usahihi wakati zoezi la kuaga likiendelea.

 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda amesema mpaka sasa jumla ya miili 18 imeshachukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya maziko wakati huo serikali ikigharamia majeneza na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Bariadi ikigharamia usafiri.

 

‘’tulikuwa na marehemu 22, miili 18 wameshachukuliwa na ndugu zao na serikali imetoa ubani kwa kugharamia majeneza..tumepata rambirambi zaidi ya shilingi mil. 6 kutoka Chama cha Wachimbaji (FEMATA) ambazo tutazipeleka kwa wafia ambapo kila mmoja atapata haki sawa’’ amesema Dk. Nawanda.

 

Dk. Nawanda amewashukuru FEMATA kwa upendo huku akisisitiza kuwa serikali itahakikisha watu hao wanahifadhiwa kwa heshima na kwamba mpaka sasa mtu mmoja hajafanikia kupata ndugu zake.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Madini Steven Masumbuko amesema wameshiriki tukio la kuwaaga wachimbaji ambapo linawakumbusha wachimbaji kuwa vitambulisho vya kidijitali ili wakipata tatizo weze kutambulika kwa haraka zaidi.

 

‘’Naawasa wachimbaji waone umuhimu wa kuwa na vitambulisho vya kidijitali ili waweze kutambulika kwa uharaka zaidi, suala la kitambulisho ni la muhimu ili kutambulika mali na uraia wetu’’ amesema Masumbuko.

 

Mwenyekiti wa FEMATA, Steven Masumbuko amewasilisha rambirambi ya shilingi Mil.6 huku akiiopongeza serikali kwa kushirikiana na wachimbaji na kuwataka wachimbaji kuendelea kufauata taratibu zinazotolewa na serikali ikiwemo Maafisa Madini wakazi.

 

MWISHO.

 

 

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa juu ya utaratibu wa kuchukua miilia ya wachimbaji waliofukiwa na udongo katika mgodi wa Ikianushu juzi.

 

 

Mwenyekiti wa FEMATA, Steven Masumbuko amewasilisha salamu za rambirambi ambapo Wachimbaji wamechangia kiasi cha shilingi Mil.6 lwa ajili ya kusaidia shughuli za mazishi ya wachimbaji waliofukiwa na udongo katika mgodi wa Ikinabushu juzi.
 
 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda akipokea rambimbari kiasi cha shilingi Mil6 kutoka FEMATA kwa ajili ya kusaidia shughuli za mazishi ya wachimbaji, katikati ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi Simon Simalenga, kulia ni Yusuph Kazi, Mwenyekiti wa Bodi ya FEMATA.

 

 

 

 

 

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم