Mhandisi Kundo aahirisha ziara Kagera, afika mgodini kutoa pole.

MBUNGE wa Jimbo la Bariadi Mhandisi Kundo Mathew (kushoto) akiongea na wachimbaji wa mgodi wa Ikinabushu wilayani Bariadi wakati akitoa salam za pole kufuatia mgodi huo kuuwa watu 22, katikati ni Waziri wa Madini Anthony Mavunde, na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda.


Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi. 


Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mhandisi Kundo Mathew ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ameahirisha ziara ya kiserikali Mkoani Kagera na kutembelea mgodi wa Ikinabushu ambao umehuo baada ya kuahirisha ziara ya kiserikali aliyokuwa akiendelea nayo mkoani Kigoma.

 

Mhandisi Kundo amewapongeza wachimbaji hao Kwa kushirikiana na Serikali kuwaopoa wachimbaji wenzao ambapo amesema Watanzania Hawawezi kutengana wakati wa shida.

 

"Nilikuwa katika ziara za kikazi, baada ya kutokea hili ilibidi niwasiliane na Waziri wa Madini ili tuje wote...tunaishukuru serikali ya Dk. Samia Kwa kuwezesha wasaidizi wake kufika maeneo ya matukio kushiriki na wananchi" amesema Mhandisi Kundo.

 

Amesisitiza kuwa atahakikisha anasimamia usalama wa wananchi wa Bariadi ikiwemo kuboresha usalama wa uchimbaji ambao wamejiajiri kupitia shughuli za uchimbaji.

 

"Mimi Mbunge wa Jimbo la Bariadi nitahakikisha gharama za usafiri wa wenzetu 22 nazigharamikia mimi mwenyewe...Naamini mimi nitaendelea kuwa upande wenu juu ya kutofunga machimbo haya ili wananchi waendelee kujipatia kipato, tuwezeshwe Miundombinu rafiki ili tuendelee kuchimba katika mgodi huu" amesema.

 

Awali baadhi ya wachimbaji wameiomba serikali kupitia Waziri wa Madini, kutofunga machimbo hayo ili shughuli za uchimbaji ziendele na waweze kujipatia vipato ikiwemo kuchangia Pato la Taifa.

 

Juma Sayi, mkazi wa Ikinabushu ambaye ni mchimbaji ameiomba serikali kusimamia ufungaji wa matimba ili mgodi huo uendelee kuzalisha kuliko kuufunga Kwa sababu watakosa kazi za kufanya.

 

Peter Malimi, Mkazi wa Dutwa ameipongeza serikali kuwafikia mara Moja kuokoa wachimbaji wenzao waliopoteza Maisha, huku akiiomba serikali kutowapatia matajiri mgodi huo ambapo wachimbaji wadogo watapoteza haki zao.

 

Naye Maria Ndimila kutoka Wilaya ya Itilima ameiomba serikali kuwaboreshea Mazingira ikiwemo ujenzi wa choo ili kuondokana na magonjwa ya milipuko ikiwemo Kuhara na kutapika.


MWISHO.

 

Waziri wa Madini Anthony Mavunde (wa pili kushoto) akisalimiana na baadhi viongozi wa Mkoa wa Simiyu kabla ya kutembelea mgodi wa Ikinabushu, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga, katikati ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mhandisi Kundo Mathew.

 


Sehemu ya shimo lililofukia wachimbaji 22 katika mgodi wa Ikinabushu wilayani Bariadi mkoani Simiyu.


Sehemu ya shimo lililofukia wachimbaji 22 katika mgodi wa Ikinabushu wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
 

 

Waziri wa Madini Antony Mavunde (wa pili kulia) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga, kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mhandisi Kundo Mathew wakia katika machimbo ya dhahabu ya Ikinabushu wilayani Bariadi wakati wakiongea na wachimbaji wamgodi huo.



MBUNGE wa Jimbo la Bariadi Mhandisi Kundo Mathew (kushoto) akiongea na wachimbaji wa mgodi wa Ikinabushu wilayani Bariadi wakati akitoa salam za pole kufuatia mgodi huo kuuwa watu 22.
 
 
 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم