Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
CHAMA cha Wanunuzi wa Pamba nchini (Tanzania Cotton Association-TCA) kimewataka wakulima wa Pamba kuhakikisha wanaongeza tija na uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya viwanda vilivyopo nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa TCA Boaz Ogolla amesema viwanda vya kuchambua Pamba vinafanya kazi chini ya kiwango kutokana na uhaba wa zao la pamba.
Amesema kiwanda cha Alliance Ginnery kilichopo Kasoli wilayani Bariadi kina uwezo wa kuchambua tani 1000 kwa mwaka na kwamba tangu wawezekeze nchini Tanzania mwaka 1998 hawajawahi kufikia hata nusu ya uwezo wa kiwanda chao.
“tangu tuwekeze tuliwahi kupata tani elfu 40, tunafanya kazi chini ya kiwango..kwa miaka mitatu iliyopita tumepanda uzalishaji ambapo mwaka 2020 tulikuwa na kilo Mil. 121, 2021 kilo mil. 144, 2023 kilo mil. 174 na mwaka huu kilo mil. 242 jambo ambalo linatupa matumaini licha ya kuwa polepole.’’ Amesema Ogolla.
Ogolla ameiomba serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo kuhakikisha wanasimamia sekta hiyo ili kuongeza tija na uzalishaji ili wakulima wapate fedha pia ajira ziongezeke.
MWISHO.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق