
Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
HIFADHI ya Taifa ya Serengeti kupitia kitengo cha ujirani mwema imeviwezesha vikundi 16 kujiinua kiuchumi kupitia utekelezaji wa miradi ya kujiongeza kipato kwa kuwapatia elimu ya uhifadhi wa mazingira, kuweka na kukopa fedha na mizinga ya nyuki.
Wanufaika zaidi ya 60 kutoka wilaya za Busega, Itilima na Meatu wamenajengewa uwezo kwa muda wa siku sita ili waweze kuendesha vikundi vitkabiliana na ujangili kwenye vijiji vinavypakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Akizungumza jana kwenye mafunzo hayo Afisa Uhifadhi kutoka Hifadhi ya Serengeti, kitengo cha Mahusiano ya Jamii, Robart Masobeji, amewataka wananchi wanaozunguka maeneo yaliyohifadhiwa kuendelea kuungana mkono jitihada zinazofanywa ili waendelee kutekeleza manufaa ya uhifadhi.
Alisema hifadhi hiyo inaendesha mafunzo ya Benki za kijamii (COCOBA) ili kuisaidia jamii kujiinua kiuchumi na kuwaongezea vipato rafiki na mazingira ambapo jumla ya mizinga 300 imewezeshwa kwenye vikundi hivyo.
‘’Tumetoa jumla ya mizinga 300 yenye thamani ya shilingi Mil. 94.5 ili kuwezesha miradi ya ufgaji nyuki, Itilima tumewapa mizinga 171 kwenye vikundi 9, Meatu mizinga 53 kwa vikundi vitatu na Busega mizingia 76 kwa vikundi vinee’’ alisema.
Alifafanua kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unatokana na manufaa ya uhifadhi, huku akiipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kutekeleza miradi hiyo.
Alizitaka jamii zinazozunguka hifadhi kuhamasika kwa kuachana na shughuli zinazolenga kuleta uharibifu katika maeneo yaliyohifadhia ikiwemo kuacha kabisa kujihusisha na ujangili ambao unakwamisha juhudi za uhifadhi.
Awali akifungua mafunzo hayo, Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka wilaya ya Busega Angela Kiama alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa miradi ya ufugaji nyuki pamoja na kutekeleza majukumu yao ikiwemo kusajiliwa kisheria chini ya uongozi wa Benki Kuu (BOT).
‘’kwa sasa tunavisajili vikundi hivyo bure katika Halmashauri zetu chini ya mpango wa huduma ndogo ya fedha katika Idara ya Maendeleo ya Jamii…tunawashauri wasijiliwe ili watekeleze majukumu yao kisheria, wafungue akaunti za benki sababu kuna wengine wana fedha zaidi ya Mil. 10 ambayo siyo rafiki kuhifadhi nyumbani’’ alisema Angela.
Aliwataka Maafisa Maendeleo ya Jamii katika wilaya za Itilima na Busega na Meatu kuwatembelea na kuwajenga uwezo ili vikundi hivyo viweze kuwa endelevu na kuwa mfano kwenye vikundi vingine ambavyo havikupata mafunzo.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka wilaya ya Meatu Lucy Sayimgunda aliwapongeza Senapa kwa kutoa mizinga ya nyuki katika vikundi vitatu vya Buzunza mizinga 19, Mkombozi mizinga 19 na Muungano Mwanyahina 15.
Alieleza kuwa vikundi hivyo vitaweza kusimamizi miradi kwa sababu vimepatiwa mafunzo na wataweza kujiinua kiuchumi na kuendeleza utunzaji wa mazingira ikiwemo kuachana na ujangili.
Aliahidi kuwa watasimamia vikundi hivyo ili viweze kuwa endelevu ili jamii nyingine iweze kuigana kuweza kujiinua kiuchumi.
Naye Vicent Elias Mkazi wa kijiji cha Mwabayanda wilaya ya Busega alisema kikundi cha Mwabayanda kwanza wamenufaika kwa kupokea mizinga 19 ambayo imeshatundikwa ili kuanza ufugaji wa nyuki.
Alisema kupitia miradi hiyo wataweza kujiongezea vipato kwa kuuza asali na mazao ya nyuki na kwamba wanaendelea kutoa elimu ili wakazi wa eneo hilo wasijihusisha na masuala ya ujangili na badaya yake wajuinge na vikundi vya ufugaji nyuki na uhifadhi wa mazingira.
MWISHO.
Post a Comment