Lucy Sabu aungana na Wanawake Watumishi kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani.

MBUNGE wa Vijana (CCM) Lucy Sabu (wa pili kulia) akimkabidhi Mashuka 50 Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Byuna Dk. Deogratius Mtaki, kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake yaliyofanyika Byuna, kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Bariadi Beatrice Gwamagobe.



Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

 

MBUNGE wa Vijana (CCM) Lucy Sabu ameungana na Wanawake Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kutembelea wagonjwa, kukabidhi mashuka 50 pamoja na mahitaji mengine kwenye kituo cha Afya Byuna.

 

Aidha, Wanawake hao pia walitembelea shula za MSingi Nkololo A’ na Ukiliguru kwa ajili ya kuongea na wanafunzi wa kike pamoja na kutoa mahitaji mbalimbali ikiwemo madaftari, Kalamu, Penseli na Taulo za kike huku wakiwasisitiza kusoma kwa bidii.

 

Awali akizungumza mara baada ya kupokea misaada hiyo, Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho Dk. Deogratius Mtaki alisema wanakabiliwa na upungufu wa wodi za wanawake kutokana na kuhudumia wananchi wengi.

 

Dk. Mtaki alimpongeza Mbunge huyo pamoja na wanawake watumishi kwa kutoa misaada ya kibinadamu pamoja na mashuka ya wagonjwa ambayo yatasaidia kupunguza uhaba.

 

‘’Mashuka haya yana nafasi kubwa sana kwetu na wagonjwa, kituo chetu kina wagonjwa wengi na tumeelewa na wagonjwa kulingana na uwezo wa eneo…tunahitaji vitu vingi viongezeke ili tuwahudumie wagonjwa kwa wakati’’ alisema.

 

Alieleza kuwa lengo la kituo hicho ni kuhudumia wakina mama 100 kwa mwezi, lakini kutokana na kuelemewa, wanahudumiwa wakinamama 160 kwa mwezi kutoka wilaya za Busega, Itilima na Bariadi.

 

Dk. Mtaki aliiomba serikali kuwaongezea jengo la wodi ya wanawake ili wawezeke kukabiliana na mapungufu yaliyopo ikizingatia kuwa serikali imeshawapatia vifaa tiba ikiwemo mashine ya mionzi (exlay) ili kuboresha utoaji wa huduma.

 

Akizungumza kwa niaba ya wanawake hao, Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Bariadi Beatrice Gwamagobe alisema wametembelea wodi ya Mama na Mtoto katika kituo cha Afya Byuna ili kusherekea pamoja baina ya watumishi wanawake na wakina mama na watoto walioko hospitali.

 

‘’Wanawake watumishi wa wilaya ya Bariadi, tumekuja na sabuni, juisi, pedi, mashuka ili kusherekea pamoja na wanawake na watoto walioko hospitali…tutaendelea kuwa pamoja nanyi muda wote’’ alisema Beatrice.

 

Kwa upande wake Mbunge wa Vijana Lucy Sabu alisema wanaendelea kuwasemea wananchi kwa serikali ili iweze kuwapatia vifaatiba na wananchi wapate huduma nzuri.

 

Alisema serikali ya Dk. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha na kuimarisha utoaji wa huduma, hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali iliyoko madarakani.

 

‘’Tumekuja na vifaa tiba (mashuka 50) kwa ajili ya kuwapatia kituo cha Afya Byuna, tumeona changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa wodi za wakina mama na watoto…tutahakikisha tunalifikisha mahali husika ili serikali iweze kuchukua hatua’’ alisema Lucy Sabu.

 

MWISHO.

 

Wanawake Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi wakiwa katika picha ya Pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Shololo, wakijiandaa kuadhimisha siku ya wanawake duniani.


Wanawake Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bariadi wakitembea kuelekeza shule ya Msingi Nkololo A' na Bukiliguru kuadhimisha siku ya Wanawake duniani ambayo hufanyika Mach 8, kila mwaka.



Mbunge wa Vijana (CCM) Lucy Sabu akifurahia jambo na kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake yaliyofanyika shule ya msingi Nkololo A'.


Mbunge wa Vijana (CCM) Lucy Sabu akikamkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nkololo A Petro Sama sehemu ya misaada  iliyotolewa na Wanawake Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kwa ajili ya Wanafunzi wa kike wa shule za Msingi Nkololo A' na Bukiliguru.




Mbunge wa Vijana (CCM) Lucy Sabu akimjulia hali Mgonjwa kwenye kituo cha Afya Byuna wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani.



 

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم