MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa
Simiyu Shemsa Seif Mohammed akizungumza kwenye Mkutano wa Tarafa kwa Tarafa kwenye Tarafa ya Nyalanja wilayani Meatu.
Na COSTANTINE MATHIAS, Meatu.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa
Simiyu Shemsa Seif Mohammed amewataka Wabunge na Madiwani kuhakikisha
wanatekeleza ahadi zao binafsi walizotoa kwa wananchi wakati wanaomba kura
kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.
Mwenyekiti huyo ametoa wito huo kwenye ziara yake
ya Tarafa kwa Tarafa katika Tarafa ya Nyalanja kata ya Mwamanongu wilayani
Meatu wakati akiongea na viongozi wa kata, mabalozi na viongozi wa dini.
Ziara hiyo inayolenga kuimarisha uhai wa Chama
pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi huku
akiwasisitiza viongozi wa kuchaguliwa kutimiza ahadi zao.
‘’Niwatake viongozi wa kuchaguliwa na wananchi,
timizeni ahadi zenu binafsi kab la hatujafika kwenye uchaguzi mkuu 2025…tekelezeni
ahadi zenu, msipotekeleza tutapata kazi wakati kuomba kura’’ alisema Shemsa.
MWISHO.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammes akisaini kitabu cha wageni kwenye mkutano wa Tarafa kwa Tarafa, katika Tarafa ya Nyalanja wilayani Meatu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed akipigiwa saluti na vijana wa Green Guard wakati akielekea kwenye Mkutano Tarafa ya Nyalanja wilayani Meatu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed
akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Meatu Fauzia Ngatumbura wakati akielekea kwenye
Mkutano Tarafa ya Nyalanja wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu Fauzia Ngatumbura (katikati) akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed (hayupo pichani) kwenye mkutano Tarafa ya Nyalanja.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed
akizungumza kwenye
Mkutano Tarafa ya Nyalanja wilayani Meatu.
Wananchi wa Tarafa ya Nyalanja wilayani Meatu Mkoani Simiyu wakifuatilia Mkutano wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed (hayupo pichani) uliofanyika kata ya Mwamanongu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed akiwa ameambatana viongozi wa CCM wakielekea kwenye mkutano wa hadhara kata ya Mwamanongu wilayani Meatu, kulia ni Katibu Mwenezi mkoa wa Simiyu Lumeni Mathias.
Wananchi wakisikiliza Mkutano wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed (hayupo pichani).
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق