*Shemsa: CCM haitabeba wagombea bali watabebwa na Matendo yao*
MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Shemsa Seif Mohamed amesema
kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu, CCM hatabeba
mtu bali atabebwa na matendo yake.
Ameyasema
hayo jana wakati akizungumza na Viongozi wa CCM wa kata, matawi,
mashina, mabalozi wa ccm, viongozi wa dini Wazee maarufu, wenyeviti wa
vijiji na viongozi na mabaraza ya jumuiya za ccm katika tarafa ya
nung'hu wilayani Maswa ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
"
tutakwenda kupitisha viongozi wa Vhama Cha Mapinduzi wanaokubalika na
Wananchi na waliowatumikia wananchi vizuri...tujikite kuwaletea wananchi
maendeleo kusikiliza kero, kutatua kero na kusimamia utekelezaji wa
ilani 'alisema shemsa.
" viongozi wangu wa
kata, tumekuwa walalamikaji badala ya kusimamia nidhamu ya CCM tumekuwa
watafuta wagombea, wa udiwani na ubunge na wao humo humo wanatafuta,
Sasa kama wewe unatafuta nafasi hiyo achia nafasi uliyo nayo ya CCM
tukupe fomu usubiri nafasi ya udiwani alisema shemsa.
"
lazima utaratibu wa chama chetu ufuatwe mnatupa kazi kubwa viongozi wa
ngazi ya Mkoa Kuja kusikiliza kero wakati ni wajibu wenu mnakaa Ofisini
kumsubiri posho kumsubiri alisema shemsa.
" tusiwachonganishe wananchi na viongozi walioko madarakani tuwaache wafanye kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi.....
MWISHO.

Post a Comment