Shemsa: CCM haitabeba wagombea bali watabebwa na Matendo yao.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohamed.

 

*Shemsa: CCM haitabeba wagombea bali watabebwa na Matendo yao*

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Shemsa Seif Mohamed amesema kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu, CCM hatabeba mtu bali atabebwa na matendo yake. 

Ameyasema hayo jana wakati akizungumza na Viongozi wa CCM wa kata, matawi, mashina, mabalozi wa ccm, viongozi wa dini Wazee maarufu, wenyeviti wa vijiji na viongozi na mabaraza ya jumuiya za ccm katika tarafa ya nung'hu wilayani Maswa ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero za wananchi.

" tutakwenda kupitisha viongozi wa Vhama Cha Mapinduzi wanaokubalika na Wananchi na waliowatumikia wananchi vizuri...tujikite kuwaletea wananchi maendeleo kusikiliza kero, kutatua kero na kusimamia utekelezaji wa ilani 'alisema shemsa.

" viongozi wangu wa kata, tumekuwa walalamikaji badala ya kusimamia nidhamu ya CCM tumekuwa watafuta wagombea, wa udiwani na ubunge na wao humo humo wanatafuta, Sasa kama wewe unatafuta nafasi hiyo achia nafasi uliyo nayo ya CCM tukupe fomu usubiri nafasi ya udiwani alisema shemsa.

" lazima utaratibu wa chama chetu ufuatwe mnatupa kazi kubwa viongozi wa ngazi ya Mkoa Kuja kusikiliza kero wakati ni wajibu wenu mnakaa Ofisini kumsubiri posho kumsubiri alisema shemsa.

" tusiwachonganishe wananchi na viongozi walioko madarakani tuwaache wafanye kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi.....
 
MWISHO.


Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم