Na Derick Milton, Bariadi.
Kiwanda cha kuchambua zao la Pamba kilichopo
katika kijiji cha Kasori Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu Alliance Ginnery,
kimetejwa kuwa kinara wa ulipaji wa Ankara za umeme katika mkoa huo.
Meneja wa Shirika la Umeme (TANESCO)
Mkoa huo Alistidia Clemence amekitaja kiwanda hicho kuwa kinara, wakati wa
mkutano wa ushirikishwaji wa wadau kwenye miradi inayotekelezwa na shirika hilo
mkoa wa Simiyu.
Alistidia amesema kuwa Alliance
Ginnery amekuwa kinara kati ya walipaji wazuri wa Ankara za umeme, huku watenja wengine
wakiwa ni kiwanda cha kuchambua pamba cha Mjini Bariadi NGS.
Meneja huyo amewataka wateja wengine
katika mkoa huo, kuhakikisha wanalipa Ankara zao kwa wakati ili kuiwezesha
Tanesco kutekeleza majukumu yake mengine ya msingi.
“ Kama TANESCO tumekuwa na majukumu
mengi na makubwa, ikiwa wateja wetu watashindwa kulipa Ankara za umeme kwa wakati
mtatufanya tushindwe kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi,” amesema Alistidia.
Alliance Ginnery na wateja wengine
ambao ni walipaji wazuri wa Ankara za umeme wamepewa vyetu pamoja na tuzo, kama
inshara ya kuwapongeza kwa ulipaji mzuri wa huduma ya umeme wanayoipata kutoka
TANESCO.
MWISHO.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق