Wenye Ulemavu na Wazee wahamashishwe kujindikisha.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shemsa Mohammed akiongea kwenye mkutano Tarafa ya Ngulyati.


Na COSTANTINE  MATHIAS, Bariadi.

 

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohammed amewataka viongozi wa ngazi zote kuhakikisha wanahamasisha Watu wenye Ulemavu na Wazee kujiandikisha katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.

 

Amesema makundi hayo maalumu yamekuwa yakiachwa nyuma kushiriki matukio muhimu jambo ambalo ni haki yao kikatiba na kwamba wanayo haki kama binadamu wengine.

 

Shemsa ameyasema hayo jana kwenye mwendelezo wa ziara yake ya Tarafa kwa Tarafa  iliyofanyika katika Tarafa ya Ngulyati, Halmashauri ya wilaya ya Bariadi kwenye kikao cha kuimarisha na kukagua uhai wa CCM.

 

Amesema watu wenye Ulemavu wa viungo, macho, masikio na wenye Ualbino wanayo haki sawa ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu baada ya kuwa wamejiandikisha na pia wanayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwa mujibu wa sheria.

 

‘’Tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji pamoja na uchaguzi mkuu, tunataka ushiriki wa watu wenye ulemavu na wazee wasiachwe nyuma, twendeni tukahamasishe wajiandikishe ili wapate sifa ya kupiga kura’’ amesema na kuongeza.

 

‘’Rais Samia ameshusha fedha nyingi na zimeenda kwa wananchi moja kwa moja, kila kijiji au kitongoji kuna mradi wa maji, umeme, barabara, zahanati au vyumba vya madarasa, fedha hizo zimegusa wanancho moja kwa moja…lazima tujiandikishe ili tupige kura kuichagua CCM’’

 

Katika ziara hiyo ya siku 16 Tarafa kwa Tarafa Mkoani Simiyu, Mwenyekiti Shemsa anakutana na viongozi wa CCM ngazi ya mashina, mabalozi, kata, wenyeviti wa vijiji na vitongoji, viongozi wa dini, kimila pamoja na wazee maarufu.

 

MWISHO.

 

Viongozi wa Shina, matawi na Mabalozi kutoka Tarafa ya Ngulyati wakimsalimia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed (hayupo pichani) kwenye mkutano ulifanyika Ngulyati sekondari.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed (kulia) akiwasalimia wajumbe (hawapo pichani) kwenye mkutano wa Tarafa kwa Tarafa uliofanyika shule ya sekondari Ngulyati, kulia ni kaimu Katibu wa CCM Mkoa huo Naboth Manyonyi, katikati ni Mzee Khamis Yusuph Balozi wa shina Ngulyati.


Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed (wa kwanza kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Bariadi Simon Simalenga, kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bariadi Juliana Mahongo.

 

 

 

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم