Makala..“NMB nondo za Pesa” Programu ilinayolenga kujibu changamoto za kifedha kwa wajasliamali, wafanyabiashara.

 


Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa nne kushoto), Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio (wa pili kulia) na Mkuu wa Huduma za Bidhaa wa Benki ya NMB, Aloyce Maro (wa tatu kushoto) wakizindua kwa pamoja Programu ya ‘NMB Nondo za Pesa’ inayolenga kutoa elimu na masuruhisho ya kifedha kwa watanzania hususani vijana na wanawake. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni baadhi ya wajasiliamali walioshiriki uzinduzi huo. 

Na Derick Milton.

 

Mwaka 2023 Shirika la Finscope linalojihusisha na masuala ya uboreshaji maisha, ustawi, na uwezeshaji wa Watanzania kupitia ushirikishwaji wa kifedha, lilifanya utafiti wa masuala mbalimbali ya kiuchumi.

 

Katika utafiti huo uligusa mambo muhimu kwa wafanyabiashara na wajasliamali wadogo wadogo ikiwemo nidhamu ya kifedha, uwekezaji pamoja na uwekeji akiba.

Utafiti huo unaonyesha uwepo wa idadi kubwa watanzania ambao wapo kwenye myororo wa ufanyaji biashara lakini hawana elimu juu ya masuala ya kifedha.

Katika eneo moja la utafiti huo, linaonyesha kuwa kati ya watu 10 wenye akaunti Benki ni mtu mmoja tu ndiye amekopa katika taasisi ambazo ni rasmi za kifedha.

 

Hali hiyo inaonyesha dhahiri kuwa kuna idadi kubwa ya watu hasa wafanyabiashara na wajasliamali wanakopa katika taasisi ambazo siyo rasmi na kupata madhara makubwa ya kiuchumi.

 

Eneo la Elimu ya kifedha linatajwa kuwa suruhisho pekee ambalo linaweza kumwinua mfanyabiashara au mjasliamali mdogo mdogo kukua kiuchumi na kukuza biashara zake.

 

Benki kuu ya Tanzania (BOT) katika miongozo yake, imeendelea kuzisisitiza taasisi mbalimbali za kifedha ambazo ni rasmi, kuwekeza zaidi katika eneo la elimu ya kifedha kwa watanzania.

 

Baadhi ya taasisi hizo za kifedha zimekuwa zikitekeleza ipasavyo miongozo hiyo, ambapo elimu imekuwa ikitolewa mara kwa mara pamoja na kuja na masuruhisho mbalimbali yanayoweza kuwainua wananchi kiuchumi.

 

Benki ya NMB Tanzania ni moja ya taasisi ambayo imeendelea kutekeleza miongozo hiyo kwa vitendo, kwani imekuwa ikitoa elimu kupitia programu na kampeini mbalimbali inayozianzisha kwa wateja wake.

 

Baadhi ya programu hiyo ni Mwalimu Spesho ambayo utoa masuruhisho mbalimbali ya kifedha kwa wakulimu, NMB Kikundi Akaunti ambayo ni maalumu kwa vikundi vya kijamii.

 

Programu nyingine ni NMB Jiwekee inayowawezesha mteja weke walioko nje ya mifumo rasmi ya ajira kujiwekea akiba, lakini pia program ya Mshiko Fasta ambapo mteja anaweza kupata mkopo usiohitaji dhamana wala ujazazi fomu.

 

Licha ya Kampeni hizo ambazo zina masuruhisho mbalimbali ya kifedha na kuwalenga zaidi wateja wake, NMB imekuja na kampeini mpya inayolenga kutoa elimu ya kifedha hasa kwa makundi ya vijana na wanawake.

 

Kampeni hiyo imepewa jina la NMB Nondo za Pesa ambayo imezinduliwa wiki hii Jijini Dar es Salaam ambapo itatekelezwa na Benki hiyo ichi nzima kupitia makongamano mbalimbali pamoja na kuhasishwa kupitia vyombo vya habari.

 

Filbert Mponzi ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB akimwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna wakati wa uzinduzi wa Kampeini hiyo..

 

Anasema kuwa NMB imekuja na programu hiyo ili kuongeza uelewa wa masuala ya kifedha kwa maendeleo na ukuaji uchumi kwa Mtanzania mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Anasema kuwa Programu hiyo ya kifedha ni endelevu ambapo walengwa ni watanzania wote, lakini kwa upekee, ikiwa na vipengele maalumu vinavyowagusa zaidi na Vijana na Wanawake.

 

Anasema kuwa kupitia NMB Nondo za Pesa, benki hiyo itakuwa inatoa elimu kwenye mada muhimu zote kuhusiana na fedha, ikiwamo namna ya kupanga bajeti, kuweka akiba, uwekezaji, mikopo, bima na mipango mingine ya kifedha.

 

“ Tunajua asilimia 66 ya watanzania ni vijana, NMB tunaona kundi hili ni muhimu sana na kwa asilimia kubwa lipo katika mnyororo mkubwa wa biashara, lakini linapokuja suala la kukuza uchumi mtu wa kwanza kuangaliwa ni mwanamke,” anasema…

 

 

“ Hata kwenye familia zetu mwanamke ndiyo nguzo kuu ya uchumi wa familia zilizonyingi, kutokana na makundi hayo kuwa muhimu, programu hii imekuja na vipengele maalumu katika kutoa elimu ya kifedha kwao,” anasema Mponzi.

 

Katika eneo la kuweka Akiba Afisa huyo wa NMB anasema kuwa bado watanzania wapo nyuma kwenye eneo hilo, ambapo benki hiyo imeona umuhimu wa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali kujiwekea akiba.

“ Unakuta mfanyabiashara anafanya kazi yake lakini hana mpango wa kujiwekea akiba kwa ajili ya kumsaidia baadaye katika mazingira yeyote, NMB kupitia programu hii tumeona hiyo ni changamoto lazima elimu itolewe,” anaeleza Mponzi.

 

Aidha katika eneo la uwezekezaji, Programu hiyo anasema imelenga kuwapa elimu wale ambao hajui fursa za uwekezaji zinapatikana wapi na unaweza kuwekeza vipi na kiasi gani cha pesa uwekeze.

“ Kuna watu wanazo pesa zao au wamekuwa wakipata pesa, lakini hawajui wapi wawezeke pesa hizo, kupitia NMB Nondo za Pesa, tumekuja na suruhisho la kuwaonyesha wale wenye nia ya kuwekeza wapi wawekeze lakini na kuwapa elimu ya umuhimu wa kuwekeza.

 

Hata hivyo NMB bado hajaliacha nyumba tatizo la mikopo umiza au mikopo kausha damu ambayo imeendelea kuwakumba wafanyabiashara au wajasliamali wadogo wadogo nchini.

 

Kampeini hii eneo la mikopo haijaliacha nyuma, kwani elimu itatolewa kwa makundi mbalimbali hasa vijana na wanawake ambao ndiyo wahanga wakubwa wa mikopo umiza na kausha damu.

Mponzi ana ainabainisha kuwa wengi ambao wamekuwa wakikubwa na mikopo umiza na kausha damu, hawana elimu ya sehemu gani sahihi wanaweza kupata mikopo kwa haraka, riba nafuu na inayoendana na biashara zao.

Anabainisha kuwa kukosekana kwa elimu hiyo, wengi wamejikuta wanakimbilia katika taasisi ambazo siyo rasmi na kujikuta wamejiunga katika mikopo ya taasisi hizo ambayo mwisho wake unakuwa mbaya.

“ NMB Nondo za Pesa imekuja na masuruhisho ya changamoto hiyo, tutatoa elimu ya umuhimu wa kukopa katika taasisi rasmi, lakini tutawaonyesha mikopo inayopatikana NMB tena yenye riba nafuu na inayopatikana kwa haraka,” anaeleza Mponzi…

 

 

Frank Silvester Mrope ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki na Bajaji (CMPD) Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam anasema kuwa ujio wa NMB Nondo za Pesa ni dawa tosha ya kutibu matatizo ya kifedha waliyonayo.

 

“NMB wamekuwa wadau wetu wakubwa, wametukopesha pesa, lakini pia vyombo vya usafiri kama pikipiki na bajaj, kwa hiyo sisi ni wanufaika wakubwa wa huduma zao na walichofanya hapa ni kutuongezea elimu zaidi za utafutaji na uwekaji akiba kwa faida yetu na vizazi vyetu,” anasema Mrope.

 

Anatoa wito kwa bodaboda na bajaji wenzake ambao wako nje ya vyama, wajitokeze kujisajili ili kuingia kwenye mifumo rasmi ya kibenki, waweze kukopesheka, kwa sababu ni ngumu kwao kupata fursa wakiwa nje ya mifumo.

 

Naye Ruth Lema Mjasliamali wa Soko la Mbezi kwa Beda, anasema kuwa uzinduzi wa NMB Nondo za Pesa umekuja na manufaa makubwa kwao kwani wamejifunza vitu vingi ikiwemo fursa za ukopaji, uwekezaji, bima na masuala mazima ya elimu ya fedha.

 

“Tumefurahia uzinduzi huu, umetuongezea vitu vingi ikiwemo namna mbalimbali za kukopa, matumizi sahihi na umuhimu wa urejeshaji wa mikopo na fursa zingine nyingi kwa vijana na wanawake. Wito wangu kwa wajasi;iamali wote kujiunga na vikundi vya kijamii na kunufaika pamoja na huduma za NMB,” anasema Bi. Ruth.

 

MWISHO.

 

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم