MastaBata la Kibabe ya NMB yatua Mwanza.

Mkuu wa Matawi na Mauzo Benki ya NMB Donatus Richard(katikati) akimpigia simu mshindi wa droo ya mwezi ya kampeni ya MastaBata La Kibabe kwenye tawi wa Kenyatta jijini Mwanza, ambapo washindi  5 wa safari ya mbuga ya mikumi, ada na Sh laki tano walipatikana.  Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Idara ya Kadi NMB Manfred Kayala na Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Winfrida Kabuje(kulia) wakishuhudia.

 



Na Derick Milton, Mwanza.


Benki ya NMB inaendesha kampeni ya ‘MastaBata la Kibabe’ kuanzia Novemba 9 mwaka huu hadi Februari 12, mwakani, ikilenga pamoja na mambo mengine, kurahisisha ulipaji ada kwa wateja wake wanaosoma au kusomesha.

 

Kiasi cha Sh. million 300 kimetengwa kwa ajili ya Kampeini hiyo, ambapo washindi wa kulipiwa ada watapokea Sh million 4 kila mmoja.

 

MastaBata la Kibabe’ inahusisha pia utoaji wa zawadi za viwango tofauti vya fedha taslimu, pamoja na kugharamia safari za mapumziko kwa washindi, kwenda katika mbuga za wanyama hapa nchini ambazo ni Mikumi na Ngorongoro, pamoja na (kwenda) nchini Dubai.

 

Ilifahamika  zaidi kwamba kila mshindi  wa kwenda mapumzikoni ana fursa ya kuchagua ama kwenda mwenza wake, ndugu au rafiki,  wote wakigharamiwa kila kitu.

 

Vigezo vya kuwa mshindi ni kutumia Kadi ya NMB kufanya malipi mbalimbali, alisema Mkuu wa Matawi na Mauzo Benki ya NMB  Donatus Richard, jana jijini Mwanza wakati wa kuchezesha droo ya kupata washindi  wa mwezi wa kwenda Mikumi, fedha taslimu shilingi 500,000 pamoja na zawadi ya kulipiwa ada hadi milioni nne.

 

“Kwa maneno mengine hii tunasema ni ‘kula bata tunakulipia ada’. Mbali na kwenda mapumzikoni au kulipiwa ada, faida nyingine ya Kampeini hii ni kupata mitaji ya biashara kupitia zawadi wa fedha taslimu, ikiwemo Shilingi 500,000 kwa kila mshindi.

 

“Lakini pia tunahamasisha matumizi ya kadi za  NMB kwa lengo la kulinda usalama wa fedha za wateja wetu. Kutembea na fedha taslimu ni gharama kwa sababu mteja anaweza kuzipoteza kwa namna yoyote ile, ikiwemo kuibiwa, “alisema na kufafanua zaidi kwamba:

 

Kigezo ni kutumia kadi ya Benki ya NMB na sio mashine ya kadi kutoka katika Benki hiyo. Hivyo, hata mteja akifika mahala ambapo hakuna mashine ya Benki, bado anaweza kulipia kwa mashine nyingine yoyote na akaingia katika droo ya kuwa mshindi wa zawadi hizo.

 

Aliongeza kwamba hadi sasa, takribani  Sh million 34.7 zimeshatolewa kwa wasindi wapatao 333, huku wateja 122 wakipokea zawadi mbalimbali za papo kwa papo.

 

Kwa ujumla, alisema, kiasi kilichotengwa kwa ajili ya kampeini hiyo kimelenga zaidi ya washindi 2,000, ambapo kila wiki washindi 100 watapokea Sh 100,000, washindi 40 zawadi za papo kwa papo, 30 watajinyakulia Sh 500,000 kila mwisho wa mwezi  kwa muda wa miezi miwili, na 10 watashinda safari za kutembelea mbuga za wanyama.

 

“Kadhalika washindi 10 watazawadiwa ada ya shule na washindi sita tiketi za kwenda Dubai kwa muda wa siku tano. Hii ndio maana halisi ya ‘MastaBata la Kibabe’, alisema.

 

Meneja mwandamizi wa Kitengo cha Kadi NMB, Manfred Mayala, aliwataka wananchi kujiunga na Benki hiyo ili kunufaika na huduma mbalimbali muhimu, ikiwemo zawadi zinazotolewa kipjndi hiki cha‘MastaBata la Kibabe’.

 

“Kila mtanzania ni mteja wetu. Cha kufanya hapo ni kujiuga na Benki yetu,” alisema.

 

Mwakili wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Winfrida Kabuje, alisema mchakato wa kuwapata washindi wa kampeini hiyo utafanyika kwa uwazi na haki, kama sheria zinavyoelekeza.

 


Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post