Na Mwandishi wetu.
VIWANDA vya Kuchambua Pamba nchini vimeanza kufanyiwa matengenezo madogo katika sehemu mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa msimu wa kuchambua Pamba 2025/2026.
Msimu wa Pamba 2025/2026 unatarajia kuzinduliwa Kitaifa kwenye mtaa wa Mwakibuga, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, Mei 2, 2025.
Aidha, Mafundi wa Viwanda vya kuchambua Pamba vya Aham Investment Co. Ltd cha mjini Shinyanga pamoja na Alliance Ginnery kilichopo Wilayani Bariadi, wanaendelea na matengenezo ili kujiandaa kuchambua Pamba katika msimu huu.
Kuzinduliwa kwa msimu wa kununua Pamba, kunaashiria kuanza rasmi kwa ununuzi wa Pamba na uchambuaji viwandani ambapo msimu huu utakuwa na Wanunuzi zaido ya 30 watakaonunua Pamba nchini.
Kwa Mujibu wa taarifa ya iliyotolewa na Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), uzinduzi huo utatoa bei elekezi ambayo itatangazwa Mei 2, 2025.
Mwisho.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق