Na Mwandishi wetu, Meatu.
WANUFAIKA wa Mikopo ya asilimia 10 ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, wamepatiwa mafunzo yenye lengo la kutumia vizuri fedha na Mikopo wanayopata ili iweze kuwanufaisha na kuongeza vipato vya familia na kukuza Uchumi wa Taifa.
Mafunzo hayo yamefanyika leo 15/04/2025 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo, huku wanufaika wakitakiaa kuzingatia nashati ya mikataba yao.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Bonji Bugeni aliyeongoza mafunzo hayo, amevitaka vikundi nufaika vya mikopo kuzingatia usimamizi mzuri wa fedha na kuzingatia masharti ya mkataba kwa kufanya marejesho kwa wakati
“fedha hizi mtakazopatiwa tunaomba zikawe chachu ya maendelo kwenu na jamii inayowazunguka, nendeni mkawe wachakalikaji mkapambane kutekeleza miradi yenu...nendeni mkawe waaminifu kwa kufanya marejesho kwa wakati na muwe na usimamizi mzuri wa fedha ili mkamilishe marejesho kwa wakati” amesema Bonji.
Mafunzo haya yameambatana na usainishaji wa mikataba baina ya halmashauri na vikundi hivyo ili viweze kutekeleza majukumu yao.
Jumla ya vikundi 39, vinavyonufaika na mkopo wa 10% ambavyo vikundi 21 ni wanawake, vikundi 14 ni vijana na vikundi 4 ni walemavu.
Halmashauri ya wilaya ya Meatu imetenga kiasi cha shilingi Milioni 263 kwa robo ya nne.
Mwisho.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Bonji Bugeni akiongea na wanufaika wa Mikopo ya asilimia 10 (hawapo pichani) katika Halmashauri ya wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com





إرسال تعليق