Na Matukio Daima App.

DAR ES SALAAM.

VIONGOZI wa zamani waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiwemo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, Benson Kigaila, wametangaza rasmi kujiondoa ndani ya chama hicho, wakisema wamechoshwa na kile walichokiita kubaguliwa na ukandamizaji wa haki za wanachama.

Wakiwa na wanachama wengine wa kundi la G-55, wakiwemo John Mrema, aliyekuwa Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi, na Catherine Ruge, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, viongozi hao walizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kueleza kwa kina sababu za kuondoka kwao.

"Sisi tumeamua wote pamoja tunajiondoa Chadema, ili tuwaachie hicho chama waendeshe wanavyotaka, chadema imeachana na malengo", alisema Kigaila.

Kwa upande wake Mwalimu ambaye alikuwa mgombea mwenza (makamu wa rais) wakati wa uchaguzi Mkuu uliopita, alikazia kwa kusema

"hatukuingia chadema kufuata vyeo, hatukuingia chadema kufuata fedha, tuliingia chadema kwa sababu tuliamini kuchangia na klupigania mageuzi ya kweli katika nchi hii".

Kuhusu hatma yao kwenye siasa za Tanzania, kundi hilo la G-55 ambalo linahusishwa na Mwenyekiti aliyepita Freeman Mbowe, ambao baadhi walikuwa sehemu ya sehemu ya Sekretarieti ya chama hicho chini ya yake wanasema hawatakwenda kujiunga na chama tagala, CCM.

Tunaondoka chadema, tutashauriana na vyama mbalimbali, tutawaambia baadaye tunakwenda wapi", alisema Kigaila na kuungwa mkono na Mwalimu ambaye alisema uelekeo sio CCM...."CCM haiwezi daarna letu".

Mpaka sasa, CHADEMA haijatoa tamko rasmi kuhusu uamuzi huo wa viongozi wake wa zamani.


Mwisho.