Na Mwandishi wetu...
Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kukubali kuanzisha majimbo mapya ya uchaguzi nane katika mikoa mbalimbali nchini huku majimbo 12 yakibadilishwa majina.
Akizungumza na wanahabari Jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025, Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Jacobs Mwambegele amesema Katika Mkoa wa Dar es salaam Majimbo mawili yamegawanywa na kuanzishwa majimbo mapya mawili ambapo Ukonga limegawanywa na kuanzishwa jipya la kivule, na jimbo la mbagala limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Chamazi.
Katika mkoa wa Dodoma, limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Dodoma mjini limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Uchaguzi la Mtumba
Katika mkoa wa Mbeya limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Mbeya mjini limegawanywa na kuanzishwa jipya la Uyole
Mkoa wa Simiyu limeanzishwa Jimbo jipya la Bariadi mjini ambapo jimbo la Bariadi limegawanywa na kupata majimbo Mawili yaani Jimbo la Bariadi vijijini na Jimbo la Bariadi mjini.
Mkoa wa Geita yameanzishwa majimbo mawili ambayo ni Katoro na Chato Kusini yakigawanywa majimbo ya Busanda na Chato.
Mkoa wa Shinyanga limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Jimbo la uchaguzi la Solwa limegawanywa na kuanzishwa jipya la Itwangi.
Kwa Sasa, Tanzania inakuwa na majimbo ya uchaguzi 272 bara yakiwa 222 na Zanzibari 50 na kata 3960 kata mpya ni 5.
Mwisho.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Jacobs Mwambegele, akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani).
إرسال تعليق