MAKALA AWASILI SIMIYU AWAKUMBUSHA WANANCHI UMUHIMU WA UCHAGUZI.

 

KATIBU wa Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makala, akiongea na wakazi wa Bariadi (hawapo pichani) kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya zamani mjini Bariadi.


Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


KATIBU wa Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makala amewasili Mkoani Simiyu katika zaira ya kukagua Uhai Chama Cha MapinduI (CCM) pamoja na kuzungumza na Wananchi katika wilaya za Busega, Bariadi na Maswa na kuwakumbusha Umuhimu wa Uchaguzi Mkuu.


Akizungumza na wakazi wa Bariadi kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Stendi ya zamani mjini humo, CPA Makala amesema Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu 2025 yamekamilika na kuwasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu yanaanzia kwa wapiga kura ambapo aliwataka kuhakiki vitambulisho vya kupigia kura na kivitunza mpaka siku ya Uchaguzi mwezi Oktoba mwaka huu.


" Maandalizi ya uchaguzi yanaanza na vitambulisho vya kupigia kura, kama mna vitambulisho vitunzeni, Uchaguzi upo kila baada ya miaka mitano...Tunawakumbusha na kuwandaa tunakwenda kwenye Uchaguzi Mkuu ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano kuchagua, Madiwani, Wabunge na Rais aambao ni lazima wachaguliwe" amesema Makala.


CPA Makala ameeleza kuwa uchaguzi ujao ni takwa la Kisheria na siyo takwa la CCM ambapo katika Uchaguzi huo vyama vya Siasa zaidi ya 18 vitashiriki Uchaguzi ikiwemo CCM huku CHADEMA wakitangaza kususia.


Amefafanua kuwa kwa Sheria hii ya Uchaguzi, imebainisha kuwa hakuna Mgombea ambaye atapita bila kupingwa, nlbali wagombea wote watapigiwa kura za ndio na hapana kwa kuzingatia mabadiliko ya Sheri ya UchaguI ambayo yamefanyika huku akisisitiza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 utafanyika.


Mwisho.























Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post