MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew, akiongea na Wananchi wa Kata ya Ikungulyabashashi kwenye Mkutano Maalumu wa kuwasilisha Utekelezaji wa Ilani ya CCM.Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew ametembelea kata ya Ikungulyabashashi na kufika katika kijiji cha Lulayu wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kwa lengo la kuwasilisha Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025.
Akizungumza kwenye Mkutano huo Maalumu, uliofanyika Shule ya Msingi Lulayu, Mhandisi Kundo amesema anatambua changamoto za Wananchi hao ikiwemo ubovu wa Barabara ya kutoka Ikungulyabashashi mpaka Lulayu pamoja ukosefu wa Shule ya Sekondari.
Amesema serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imeeendelea kutekeleza miradi ya Maji, Elimu, Afya, Umeme na kwamba wananchi wanatakiwa kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kumpatia kura za kishindo kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.
"Kwa kutambua jitihada za Serikali, nimeleta na nitakabidhi bati ili kukamilisha upauaji wa vyumba vya madarasa, pia Rais Dk. Samia amenipa fedha za kununua pampu za Maji ambazo kila Kijiji kitapata pampu moja" amesema Mhandisi Kundo.
Katika kutimiza ahadi ya akina mama kwenye sekta ya Maji, Mbunge huyo amesema ameleta pampu nne ambapo kila pampu inagharimu shilingi Mil. 3.5 huku vijana wakikabidhiwa mipira na jezi.
"Lulayu tunakabidhi mabati 156, Mkuyunji mabati 104 na Mwahalaja mifuko 50 ya saruji...Lulayu tunawapa mipira minne na pea moja na jezi, Ikungulyabashashi mipira minne na jezi pea 1, Mkuyuni Mipira minne na jezi pea moja na Mwahalaja mipira minne jezi pea moja" amesema.
Mwisho.
![]() |
![]() |









Post a Comment