Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Wananchi wengine kumpigia kura Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2025 ili aendelee kuwatumikia na kuwaletea Maendeleo.
Mhandisi Kundo ameyasema hayo leo kwenye Mkutano Maalumu wa kuwasilisha Ilani ya CCM 2020/2025 uliofanyika kata ya Sapiwi ambapo alisema CCM imempitisha Rais Dk. Samia kugombea nafasi ya Urais.
"Siku ya Uchaguzi Mkuu, tujitokeze Kwa wingi kumpigia kura Rais Dk. Samia Suluhu Hassan sababu amepitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM kugombea nafasi ya Urais...tumpigie kura ili aendelee kututumikia" amesema Mhandisi Kundo.
Amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imetekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika kata ya Sapiwi ikiwemo ujenzi wa Zahanati, chuo cha IFM, miradi ya Umeme pamoja na ujenzi wa Barabara ili kuwarahisishia huduma wananchi.
Post a Comment