MHANDISI KUNDO AWASILISHA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM.

 

MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew akiwa ameshika begi lenye Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025.


Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew amewasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025 ikiwa ni kielekezo cha Miradi ya Maendeleo iliyofanyika ndani ya miaka mitano.


Katika taarifa yake kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM wilaya ya Bariadi, Mhandisi Kundo amesema kuwa katika muda wa miaka mitano serikali imetekeleza miradi katika sekta ya Elimu, Afya, Maji, Umeme na Barabara pamoja na kuboresha senta za vijiji kwa kuweka taa za Barabarani.


"Ndani ya miaka mitano yamejengwa madaraja 45, kwenye senta za vijiji vya Nkololo, Nyangokolwa, Dutwa, Sapiwi na Ngulyati kuna taa za Barabarani, minara 42 imejengwa kuboresha masiliano" amesema na kuongeza.


"VETA Bunamhala umegharimu Shilingi Bil.5, tumejenga visima vya Maji na kuwahakikisha wananchi upatikanaji wa Maji safi na salama, tumeanzisha ujenzi wa Ofisi za CCM za kata na kuwapatia usafiri viongozi wa Kata...nawashukuru Kwa kuniamini na kusimamia miradi ya Maendeleo katika Jimbo la Bariadi" 


Mwisho.












Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post