ITILIMA YAANZA KUTOA MIKOPO KWA KUTUMIA MFUMO JUMUISHI WA KIBENKI.

 



Na Mwandishi wetu, Itilima.


HALMASHAURI ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, imeweka Historia  kuwa Halmashauri ya kwanza kuanza kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa kutumia mfumo jumuishi wa Kibenki.


Halmashauri hiyo imetoa Mkopo wa shilingi Mil. 117 kwa Vikundi 15, ikihusisha Vikundi 6  vya wanawake, Vikundi 6 vya Vijana na Vikundi vitatu vya Jamii ya watu wenye ulemavu.


Halmashauri ya Itilima ni miongoni mwa Halmashauri 10 za Mfano zilizochaguliwa na serikali kuanza kutoa mikopo hiyo kwa Mfumo jumuishi wa Kibenki baada ya huduma hii kurejeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa imefanyiwa maboresho.


Mmmoja wa wanufaika wa vikundi hivyo, Marimu Malase anasema amewahi kunufaika na mkopo wa serikali kwa kukopa kiasi cha Shilingi Mil.8 na kurejesha kwa wakati ambapo amewasisitiza wanufaika wengine kuzingatia masharti ya fedha hizo. 


Mwisho.






Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم