MBUNGE AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KUIUNGA MKONO SERIKALI



Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi. 


MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew amegawa vifaa vya Michezo ikiwemo jezi na Mipira katika kata ya Kasoli wilayani Bariadi Mkoani Simiyu ili kuiunga mkono serikali katika sekta ya michezo. 


Akizungumza kwenye mkutano maalumu wa kuwasilisha Ilani ya CCM (2020/2025), Mbunge huyo amesema anatambua jitihada za serikali ya Rais Dk. Samia katika kuinua sekta ya michezo kwa kusapoti michezo ya kimataifa kupitia Goli la Mama. 


"Nakabidhi jezi na mipira ili kuunga mkono jitihada za serikali katika kuinua sekta ya michezo, tumeona Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anavyosaidia michezo kupitia goli na mama... Na Mimi nawaunga mkono ili tupate vijana wazuri kuanzia ngazi ya vijij waweze kucheza kimataifa" amesema. 


Kwenye kata ya Kasoli, Mbunge huyo amekabidhi mipira 14 na jezi pea tano kwa ajili ya vijiji vya Nduha, Kasoli, Mwamlapa na Busese ambapo Kila kijiji kitapata mipira mitatu na jezi pea moja huku kata ya kasoli ikikabidhiwa mipira miwili na jezi pea Moja na pampu Moja Moja kwa kila Kijiji.


Mwisho.






Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم