Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha, (kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita.
Na Mwandishi wetu, Maswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha, leo 9 Agosti, 2025 ameupokea Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Njiapanda Wilayani Maswa Mkoani Simiyu ukitokea Mkoani Shinyanga.
Macha ameupokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita tayari kwa kuukimbiza katika Halmashauri sita za Mkoa wa Simiyu ambazo no Maswa, Meatu, Itilima, Bariadi Mji, Bariadi Vijiji na Busega.
Ukiwa Mkoani Simiyu Mwenge wa Uhuru utazindua, kufungua, kuweka mawe ya Msingi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 25.9.
Mwisho.



إرسال تعليق