WAKULIMA SIMIYU, MARA NA SHINYANGA WASISITIZWA KUTUMIA TEKNOLOJIA KUONGEZA UZALISHAJI.

 

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Mtambi akikagua vipando kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.


Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


SERIKALI imewataka Wakulima, Wafugaji na Wavuvi kutoka Mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga kuhakikisha wanatumia Teknolojia na mbinu za kisasa katika shughuli za uzalishaji ili kuongeza tija ya mazao wanayozalisha kwa lengo la kupata soko la uhakika.


Aidha, wametakiwa kutumia vizuri maonyesho ya Wakulima Nanenane yaliyofanyika katika Kanda mbalimbali nchini huku wakisiisitizwa kutumia vizuri Elimu inayotolewa na wataalamu wa sekta hizo.


Hayo yamebainishwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Mtambi wakati akifunga maonyesho ya wakulima Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.


Amesema kuwa shughuli za kilimo, Mifugo na Uvuvi zikifanyika kwa kutumia Teknolojia za kisasa zitaongeza tija na kwamba Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia imefungua fursa kwenye sekta zote za ikiwemo Mifugo kwa kuanzisha sera rasmi ya Mifugo.


"Tuitumie vizuri maonyesho haya kujifunza, tulime, tufuge na kuvua kwa kufuata taratibu, tumeomba tija ni kubwa...tuache Ufugaji wa kizamani na tufuge kisasa tutapata faida kubwa" amesema Kanali Evance.



Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wafugaji kuhakikisha Mifugo yao inapata chanjo ili kudhibiti magonjwa ya mifugo huku akiwasisitiza Wafugaji kurasimishwa sekta ya Mifugo na kuwataka changamkieni fursa ya ufugaji wa kisasa.


Awali Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha amesema kuwa Wananchi zaidi ya elfu name  wamefika kwenye  maonyesho ya Nanenane kujifunza na kupata elimu ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi wa kisasa.



Kwenye Kilimo, Macha amesema kuwa serikali imejikita kufanya Kilimo chenye tija hasa Kilimo cha umwagiliaji ambacho ni Kilimo Cha uhakika huku akiwasisitiza wakulima kwenye maeneo yenye fursa za umwagiliaji wajiunge kufanya Kilimo kinachozingatia mbinu na tija.


Mwisho.







Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم