Wafanyakazi Wanawake wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu, wamesherehekea Siku ya Wanawake duniani kwa kutoa zawadi mbalimbali katika makundi mbalimbali ya jamii yanayozunguka mgodi huo.
Akiongea katika hafla ya maadhimisho hayo, Meneja wa mgodi huo Cheick Sangare, amesema kuwa kampuni itaendelea kutekeleza sera yake ya kuhakikisha wanawake wanapatiwa fursa sawa na wanaume na aliwataka wajiamini na kuendelea kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya uchimbaji wa madini.
Meneja wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Cheick Sangare, akiongea na wafanyakazi Wanawake wa mgodi wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Kaimu Meneja Mahusiano ya jamii Zuwena Senkondo, akiongea wakati wa hafla hiyo.
Wafanyakazi Wanawake wa Barrick Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
Viongozi wa Barrick na baadhi ya madiwani wa vitongoji vinavyozunguka mgodi wakati wa hafla hiyo
Meneja wa Barrick Bulyanhulu,Cheick Sangare, akitoa cheti kwa Wanawake wanaoendesha mitambo wakati wa hafla hiyo.
Wafanyakazi walipata fursa ya kutembelea shule ya sekondari ya Mwingilo na kuongea na wasichana wa shule hiyo sambamba na kuwapatia zawadi za taulo za kike.
Wafanyakazi walipata fursa ya kutembelea shule ya sekondari ya Mwingilo na kuongea na wasichana wa shule hiyo sambamba na kuwapatia zawadi za taulo za kike.
إرسال تعليق