Na Bahati Sonda, Simiyu.
Imeelezwa kuwa watu 71 hupoteza maisha kila siku hapa nchini kutokana na ugonjwa wa kifuu kikuu (TB) sawa na 25,000 kwa mwaka.
Hayo yameelezwa jana mjini Bariadi na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu duniani mwaka huu ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Simiyu.
Amesema kuwa serikali inapambana na Ugonjwa huo kwa kusaidiana na Wadau mbalimbali wa Afya hapa nchini.
Waziri Ummy amesema kuwa Ugonjwa huu unatibika na hivyo kuwaomba watu wote wenye dalili za Ugonjwa huo kufika katika Vituo vya Afya kwa ajili ya uchunguzi wa Ugonjwa huo na watakaogundulika wataanzishiwa matibabu.
Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo amesema kuwa ugonjwa huo ni hatari sana na hupelekea kupunguza kwa nguvu kazi ya jamii hali inayosababisha kushindwa kufanya maendeleo yao binafsi pamoja na kuchangia pato la Taifa.
Amebainisha kuwa ugonjwa huo bado ni janga kubwa na kwamba asili36ya vifo vya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi husababishwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu.
Katika hatua nyingine ameitaka Wizara zote ambazo ziko katika hatari ya kupata maambukizi ya Kifua Kikuu ikiwemo Wizara ya Madini kuhakikisha mikakati ya kukubaliana na ugonjwa huo kwani wachimbaji wengi wadogo wapo katika hatari ya kupata maambukizi.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda amesema kuwa wagonjwa 3689 waliotibiwa na kupona ni asilimia 99 ya wagonjwa wote.
Mwisho.
Post a Comment