Wenye maisha Duni, wako kwenye hatari zaidi kupata TB.

 


Na Derick Milton, Simiyu.


Watu wanaoishi kwenye maisha duni (umaskini) wanatajwa kuwa katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa Kifua kikuu, kutokana na hali zao za kimaisha kutozingatia masharti ya kujikinga na ugonjwa huo.


Mbali na hilo, watu wenye tatizo la utapiamlo hasa watoto nao wanatajwa zaidi kuwa kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo.


Mratibu wa mapambano dhidi kifua kikuu kutoka Muungano wa wadau wa kupambana na ugonjwa huo Nelson Telekera, wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoa wa Simiyu juu ya Ugonjwa huo.


Amesema kuwa watu wenye hali ya chini kimaisha, wako kwenye hatari zaidi kutokana na mfumo wa maisha yao ya kila siku hasa nyumba ambazo wamekuwa wakiishi kutoruhusu upitaje wa hewa kwa urahisi.


Anasema kuwa asilimia kubwa ya wananchi ambao wanaishi vijijini wengi wao wamejenga nyumba zenye madirisha madogo, ambayo hayawezi kupitisha hewa ya kutosha.


“ Ikiwa ndani atakuwemo mtu mwenye kifua kikuu, basi ni rahisi kuwaambukiza wengine kwa sababu hakuna hewa ya kutosha inatoka na kuingia na tunajua ugonjwa huu unaambukizwa kwa njia ya hewa” amesema


“ kutokana na mfumo wa madirisha madogo kutoruhusu hewa kuingi na kutoka, kama kuna mtu ndani ana maambukizi basi wadudu watakaa humo ndani na wataweza kuambukizwa watu wengine,”


Aidha pia amesema kuwa mara nyingi watoto wenye utapiamlo wengi wao wanapokwenda kupima, lazima wakutwe na tatizo la Kifua kikuu, hivyo mtu mwenye utapimlo ni rahisi kupata ugonjwa huo.


“ Tunajua matatizo ya lishe nayo utokea kwenye familia duni, hasa utapiamlo kwa watoto wadogo, mara nyingi mtu mwenye tatizo hilo yuko kwenye hatari kubwa sana ya kupata ugonjwa wa kifua kikuu,”


Amewataka wananchi kuchukua tahadhari, kwa kuhakikisha nyumba wanazojenga zinakuwa na madirisha makubwa yanayoweza kupitisha hewa na mwanga wa kutosha kila wakati.


“ Tunawashauri pai wananchi kuhakikisha wanakula vyakula vya makundi yote ya lishe, ili kuhakikisha wanakuwa na kinga za kutosha za kuweza kupambana na ugonjwa huo,” amesema.


MWISHO.



Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post