Thomas Nkola; Aibuka za Sakata la Bandari, awataka wenye maoni waishauri serikali.

Katibu wa Nyanda za Malisho, Migogoro ya Wafugaji na Watumiaji wengine wa ardhi kutoka Chama cha Wafugaji Tanzania Thomas Nkola akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), kushoto ni Paul Basu Mkazi wa Malampaka. 


 Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

 

THOMAS Nkola maarufu Mkulima aliyetikisa hivi karibuni baada ya kufungua kesi katika Mahakama ya Kisutu kuhusu ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ili viongozi waliotumia madaraka vibaya wawajibishwe, ameibukia Sakata la Bandari akiwataka wenye maoni waishauri serikali na siyo kutoa waraka au kurumbana kwenye mitandao ya kijamii.

 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bariadi jana, Nkola amewataka Viongozi wa Dini, Vyama vya Siasa na Wananchi kutoa maoni na kuishauri serikali kuhusu Mkataba wa uwekezaji wa Bandari ili kujenga nchi kwa pamoja.


Aidha, wametakiwa kutayarisha kasoro za Mkataba wa Bandari ili wakakae meza moja na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya marekebisho kwa lengo la kuboresha uwekezaji ambao utaongeza ajira na kukuza uchumi wa taifa.

 

Nkola ambaye pia ni Katibu wa Nyanda za Malisho, Migogoro ya Wafugaji na Watumiaji wengine wa ardhi kutoka Chama cha Wafugaji Tanzania, amesema chama cha Wafugaji kinaunga mkono uwekezaji wa Bandari.

 

Nkola amewataka viongozi wa dini, vyama vya siasa na wananchi kutumia busara kubainisha kasoro za mkataba wa Bandari kwa manufaa ya taifa ili kila mmoja anufaike na Rasilimali za Taifa.

 

‘’Namwomba Mheshimiwa Rais Samia, afanyie kazi kasoro zilizomo kwenye mkataba kama zinavyoainishwa ili pande mbili wazione zinafaa na maisha yaendelee…sisi wakulima na wafugaji hatuna tatizo na mkataba huu isipokuwa tunaomba yafanyiwe kazi marekebisho na mapungufu ya mkataba kama tunavyoyasikia kutoka sehemu tofauti tofauti’’ amesema Nkola.

 

Nkola almaarufu Mkulima ambaye anajiita mzalendo, alijizolea umaarufu baada ya kufungua kesi Mahakama ya Kisutu kuhusu ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) baada ya kumwona Rais Samia akikasirishwa na ripoti hiyo ili viongozi waliotajwa wawajibishwe kwa mujibu wa sheria kutokana na matumizi mabaya ya madaraka.

 

MWISHO.

 

 

Katibu wa Nyanda za Malisho, Migogoro ya Wafugaji na Watumiaji wengine wa ardhi kutoka Chama cha Wafugaji Tanzania Thomas Nkola akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), kushoto ni Paul Basu Mkazi wa Malampaka.  
 

 




 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم