CCM yaiekeleza Serikali kukamilisha Maboma Sekta za Elimu na Afya.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed (wa pili kulia) akikagua ujenzi wa shule ya Sekondari Mbugabanhya, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda.

 


Na COSTANTINE MATHIAS, Meatu.

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu kimeitaka serikali kutenga bajeti ili kukamilisha maboma ya zanahati, vyumba vya madarasa, nyumba za walimu ambazo zimejengwa kwa nguvu za wananchi.

 

Hayo yamesema leo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo, Shemsa Mohammed wakati akiongea kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Mbugabanhya na Mwandu Itinje wilayani Meatu katika ziara ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM.

 

Amesema licha ya serikali kuendelea kutekeleza miradi mingi ya maendeleo katika sekta za Elimu na Afya, watendaji wanatakiwa kuendelea kutenge bajeti ili kukamilisha majengo yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi.

 

‘’Pitieni Maboma yote yaliyojengwa kwa nguzu za wananchi ili myakamilishe, tengeni bajeti ili wananchi waone tija ya michango yao kuliko kuyatelekeza na kuanza ujenzi mpya’’ amesema na kuongeza.

 

‘’Rais Samia anatoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya, Zahanati, Shule za Msingi na Sekondari, Maabara na Mabweni lakini katika maeneo yetu kuna majengo yalichangiwa kwa nguvu za wananchi na hayajakamilika…tengeni bajeti kuyakamilisha.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda amemhakikishia Mwenyekiti huyo kuwa watashirikiana na Halmashauri kuhakikisha wanatenga bajeti ili kukamilisha maomba hayo.

 

Akiwa wilayani Meatu, Mwenyekiti Shemsa amekagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari Mbugabanhya inayotekelezwa kwa gharama ya shilingi Mil. 584 kupitia Mradi wa SEQUIP.

 

Pia amekagua ujenzi wa shule ya mpya ya msingi Mwandu Ikindilo inayotekelezwa kupitia mradi wa BOOST kwa gharama ya shilingi Mil. 540 na kuipongeza serikali kwa kutoa fedha pamoja na usimamizi mzuri wa watendaji katika miradi hiyo ambayo imeonyesha thamani halisi ya fedha.

 

MWISHO.

 

Shule ya Msingi Mwandu Ikindilo iliyojengwa kwa gharama ya shilingi Mil. 500.

 

Viongozi wa CCM wakikagua ujenzi wa shule ya Msingi Mbugabanhya.
 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed (wa pili kulia) akikagua ujenzi wa shule ya Sekondari Mbugabanhya, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda.
 
 
Viongozi wakitembelea ujenzi wa shule ya Mpya ya Sekondari Mbugabanhya inayojengwa kupitia Mradi wa SEQUIP.
 
Viongozi wa Chama na Serikali wakizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwandu Itinje.
 

Darasa jipya la Awali shule ya Msingi Mwandu Ikindilo lililojengwa kupitia mradi wa BOOST.
 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed (katikati) akitembelea mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya Msingi Mwandu Ikindilo, kulia ni Katibu wa CCM Mkoa huo Eva Ndegeleki, kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa huo Koga Machupa.
 

Viongozi wakikagua vyumba vya madarasa shule ya Msingi Mwandu Ikindilo wilayani Meatu Mkoa wa Simiyu.
 

Vyumba vya Madarasa shule ya Msingi Mwandu Ikindilo wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu.
 
 

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم