KIFO cha Papa kinaanzisha mchakato maalum uliojaa taratibu za muda mrefu desturi ambazo huashiria nyakati kuanzia kifo cha Papa, mazishi yake, hadi mwanzo wa Conclave na uchaguzi wa mrithi wake.
Lakini ni nini hasa hufanyika ndani ya Vatican wakati wa kipindi cha Sede Vacante (yaani “Kiti Tupu”)?
Mara tu Papa anapofariki, wakuu wote wa Idara (Dicasteries) za Curia ya Kipapa wanawasilisha barua zao za kujiuzulu, isipokuwa wale wachache walioteuliwa kuendelea ili kuhakikisha shughuli za kawaida za Vatican haziathiriki.
Baraza la Makardinali (College of Cardinals) ndilo linaendelea kuwa chombo pekee chenye mamlaka ya kumchagua Papa mpya, kwa kuzingatia mila ya karne nyingi iliyowekwa katika kanuni za sheria za Kanisa (kanuni za kanisa katoliki).
Kufikia tarehe 21 Aprili 2025, Baraza hilo lilijumuisha Makardinali Wapiga Kura 135, ambapo 108 kati yao waliteuliwa na Papa Francis, na wengine 117 walikuwa Makardinali wasiokuwa wapiga kura (kwa sababu ya umri au sababu nyingine).
Makardinali waliokwisha timiza miaka 80 siku ya kuanza kwa Sede Vacante hawaruhusiwi kushiriki katika upigaji kura. Hata hivyo, bado wanaweza kushiriki katika mikutano ya maandalizi inayoitwa Kongamano Kuu (General Congregations).
Ili Papa mpya achaguliwe kihalali, ni lazima apate kura ya theluthi mbili ya wapiga kura waliopo. Ikiwa idadi ya wapiga kura haiwezi kugawanyika kwa tatu bila baki, kura ya ziada inahitajika.
Baada ya uchaguzi kufanyika, Mkuu wa Baraza la Makardinali (Dean of the College) humuuliza aliyeshinda kwa niaba ya wote:
“Je, unakubali kuchaguliwa kwako kihalali kuwa Khalifa wa Mtakatifu Petro?”
Na akijibu kwa kukubali, huulizwa:
“Unataka uitwe kwa jina gani?”
Majukumu ya mthibitishaji (notary), kwa ushuhuda wa Maafisa wawili wa Ceremonia, hutekelezwa na Mkurugenzi wa Sherehe za Kiliturujia za Kipapa, ambaye huandika hati rasmi ya kukubali uchaguzi huo na jina jipya alilochagua.
Kuanzia wakati huu, aliyeteuliwa anapata mamlaka kamili na ya juu kabisa juu ya Kanisa la Ulimwengu mzima. Conclave hukamilika papo hapo.
SOURCE.
#StarTv.
إرسال تعليق