Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.
MWENYEKITI wa UVCCM Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (MCC), Mohamed Kawaida amewataka wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura ili wawe na sifa ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa Viongozi.
Akiwa kwenye Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kashishi wilayani Itilima Mkoani Simiyu jana, Kawaida amewasisitiza wananchi juu ya Umuhimu wa kujiandikisha ili wapige kura kwenye Uchaguzi utakaofanyika mwezi Oktoba 2025.
"Tujitokeze kwa kujiandikisha ili tuwe na sifa ya kuchagua na kuchaguliwa...vijana nawatia shime mjitokeze kuwania nafasi za uongozi kwenye Ubunge na Udiwani" amesema Kawaida.
Awali Mbunge wa Itilima, Njalu Silanga aliwataka wananchi kutambua Maendeleo yaliyofanywa na CCM katika Jimbo hilo huku akiwasisitiza kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anayetekeleza miradi ya Maji, Umeme, Elimu, Afya na ujenzi wa miundombinu mingine.
Njalu pia akiwasisitiza wananchi kuwaunga mkono viongozi wanaotokana na CCM ili washirikiane na Rais kuwaletea Maendeleo katika maeneo yao.
Mwisho.

إرسال تعليق