BEI YA PAMBA KUTANGAZWA KESHO MWAKIBUGA.


 

Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


SERIKALI kupitia Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), inatarajia kutangaza Bei elekezi ya Pamba katika msimu wa kilimo 2025/2026, kesho Alhamisi, Mei 2, 2025 kwenye mtaa wa Mwakibuga Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


Macho na masikio ya Wakulima wa Pamba kutoka mikoa zaidi ya 17 nchini inayolima zao hilo, wanatarajia kupata mwelekeo wa bei dira ya zao la Pamba.


Katika msimu wa 2024/2025, Bodi ya Pamba ilitangaza bei elekezi ya shilingi 1,150/= kwa kilo moja ya Pamba daraja la kwanza na daraja la pili ikiwa ni shilingi 575/= kwa kilo moja.


mwisho.




Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم