CCM KUZINDUA ILANI YA UCHAGUZI 2025/2030.

 

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amosi Makalla, akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani).


Na Mwandishi wetu.


KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amosi Makalla, leo tarehe 17 Mei 2025 amezungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM Lumumba Dar es Salaam ambapo ametangaza rasmi tarehe ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kuwa ni tarehe 29-30 Mei 2025 jijini Dodoma.


CPA Makalla pia ametumia nafasi hiyo kutaja agenda za mkutano mkuu ambazo ni;


1. Kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya kipindi cha miaka mitano 2020- 2025 ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali Mapinduzi ya Zanzibar.


2. Kupokea na Kuzindua Rasmi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025- 2030


3. Kufanya marekebisho katika Katiba ya Chama cha Mapinduzi (CCM).


Mwisho 



Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم